IDADI NDOGO YA WASHIRIKI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO YAONGEZEKA KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 10 NCHINI
Idadi ya washiriki wa kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini
Tanzania imeonekana kuwa na idadi ndogo iliyoongezeka katika kipindi cha
miezi 10 iliyopita.
Takwimu zilizotolewa mwaka huu na makao makuu ya kanisa hilo
katika maeneo yake mawili ya kiutendaji hapa Tanzania yaani Unioni Konferensi
ya Kaskazini na Unioni ya Kusini zinaonesha kuwa Unioni ya Kaskazini yenye
konferensi nne mpaka kufikia mwishoni mwa robo ya pili ya mwaka 2014 ilikuwa na
washiriki 336,305 na ile ya kusini yenye konferensi mbili ina washiriki
104,348.
Hii inamaanisha kwamba kuna washiriki wa kanisa hilo kwa sasa
wapatao 440,653 kati ya watanzania zaidi ya milioni 40 kwa mujibu wa takwimu hizo
ambalo ni ongezeko la washiriki 29,362
katika kipindi cha miezi 10 toka disemba
mwaka jana.
Takwimu zilizotolewa na Uongozi wa Kanisa hilo Disemba
mwaka jana zinaonesha kulikuwa na washiriki wa kanisa hilo wapatao
322,351 katika Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania na washiriki 88,940
katika Unioni ya kusini mwa Tanzania hii ni kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa
na uongozi wa kanisa hilo nchini.
Hata hivyo utafiti unaonesha kuwa makanisa mahalia yamekuwa
yakishindwa kutoa malezi ya kiroho na kuratibu
idadi kubwa ya washiriki wapya wanaoongezeka kutokana na mikutano mbalimbali ya
injili inayofanyika nchini ambapo jumla ya watu 35,657 walibatizwa katika
kanisa hilo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka jana na hivi
karibuni huko jijini mwanza walibatizwa watu 3000
Kanisa la Waadventista Wa Sabato duniani lina waumini milioni
18 katika nchi 215 zilizopo kwenye
divisheni 13 za kanisa hilo.
Post a Comment