LHRC-YAWAOMBA WANANCHI WA TANZANIA KUUNGA MKONO KUPINGA ADHABU YA KIFO
Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu nchini kimewaomba wananchi kuunga mkono
jitihada za kituo hicho katika kupinga adhabu ya kifo kwani adhabu hiyo
inakwenda kinyume na haki za binaadam lakini pia kuvunja sheria ya haki ya mtu
ya kuishi.
Akizungumza
na Morning Star Radio katika kipindi cha Jamii yetu jana , Mwanasheria
kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam Bi. Benadetha Thomas amesema kuwa,
kituo cha sheria na haki za binadamu kinapinga adhabu ya kifo kwasababu wakati
mwingine mtuhumiwa anakuwa hajafanya kosa hilo na inapogundulika tayari hukumu
ya kifo inakua imeshatekelezwa.
Mwanasheria
huyo amesema kwa kipindi chote cha awamu mbili za Rais wa awamu ya tatu na
awamu ya nne haijawahi kutekelezwa ingawa tayari hukumu za adhabu ya kifo
zimeshatolewa na wafungwa zaidi ya 364 wapo kwenye magereza mbali mbali nchini
lakini hawajui lini hukumu zao zitatekelezwa.
Thomas
ameyasema hayo ikiwa zimebaki siku 4 ili kuweza kuadhimisha siku ya kupinga
adhabu ya kifo duniani ambayo hufanyika October 10 kila mwaka, huku kituo cha
sheria na haki za binaadamu kikijipanga kwa ajili ya kutoa Tamko ili kupinga adhabu hiyo hapa nchini.
Post a Comment