MTANGAZAJI

RAIS KIKWETE AMTEUA MKURUGENZI WA MASHITAKA MPYA

Picha kwa Hisani ya Mroki Blog
 
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga (Pichani Katikati) kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.
 
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, jana Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.

 
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Oktoba, 2014.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.