SENGEREMA:UNESCO YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA REDIO JAMII
Meneja
wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza
Bw. Felician Ncheye, akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kwa
washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo
katika masuala ya masoko na Tehama kwa mameneja na waandishi wa habari
takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, yanayoendelea kwenye
kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema
litaendelea kusaidia kuimarika kwa redio za jamii nchini kwa kuwa ndio
nyenzo muhimu za maendeleo ya wananchi kwa kuwapa sauti katika huduma na
shughuli zao.
Kauli
hiyo imetolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa mameneja
na watendaji takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, mafunzo
yanayofanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema FM.
Katika
mafunzo hayo watendaji hao watafunzwa masuala ya Tehama na utafutaji wa
soko kwa lengo la kufanya redio hizo kuwa endelevu na kujiendesha
zenyewe kwa kuweza kutekeleza miradi yake na kuendelea kushirikiana na
wananchi.
Mafunzo
hayo ni utekelezaji wa mradi wa miaka mitatu wa kuwezesha redio za
jamii nchini unaoendeshwa na UNESCO baada ya redio hizo nyingi
kusaidiwa kuanzishwa katika miaka ya karibuni.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akizungumza na Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio tisa za
jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika
masuala ya masoko na matumizi ya Tehama yanayofadhiliwa na mradi wa
SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na
Utamaduni (UNESCO). Kushoto mgeni rasmi Ofisa mdhani kutoka Wizara ya
Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya
usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed.
Kwa
mujbu wa Yusuph mradi wa SIDA ambao umekuwa ukitekelezwa kwa kipindi
cha miaka mitatu umeshughulika na uboreshaji wa redio hizo ili
kuzipatia uwiano na pia kuziwezesha kutumia Tehama kuhabarisha wananchi
pia kutokana na mafanikio yaliyopatikana mradi huo utaendelea kwa miaka
mingine mitatu.
Ametaja
mafanikio hayo kuwa yamepatikana kwa ushirikiano wa Redio za jamii
pamoja na shirika hilo hali iliyofanya kuyavuta mataifa mengine
kuchangia kwa ajili ya kuendelea kuzijengea uwezo redio za jamii kupitia
shirika hilo.
Ameongeza
kuwa kufanikiwa kwa redio za jamii nchini Tanzania katika mradi huu wa
SIDA kumefanya mashirika mengi yanayotaka kufanyakazi na wananchi wa
kawaida kukimbilia UNESCO kutambua redio za jamii ambazo zinaweza
kufanyakazi nayo.
Mradi
huo wa Tehama unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na
kuratibiwa na UNESCO ni sehemu ya mradi wa UNESCO katika nchi saba za
Afrika , Tanzania ikiwamo.
Baadhi
ya Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali za jamii
wakimsikiliza Bw. Al Amin Yusuph kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo
yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema
Telecentre mkoani Mwanza.
Katika
mafunzo hayo yanayofanyika mjini Sengerema, elimu inatolewa kwa wakuu
wa vituo na waandishi wa habari kutoka redio Micheweni FM, Orkonerei FM,
Pambazuko FM, Mtegani FM, Kahama FM, Redio FM, Kyela FM, Fadeco Radio
na Pangani FM.
"Kuna
mambo mengi yamefanikiwa.. kikubwa zaidi kumpa nafasi mwananchi
kujieleza na kueleza matumaini yake.." alisema Yusuph ambapo aliongeza
kwamba kutokana na mradi huo kufanikiwa zipo nchi na mashirika ambayo
yapo tayari kuchangia uimarishaji wa redio za jamii nchini.Hakuzitaja
nchi hizo.
Alisema
kutokana na mafanikio yaliyopo ya redio hizo kuwa karibu na jamii,
SIDA kwa kushirikiana na UNESCO wametengeneza programu hiyo ili
kuwezesha kuwepo kwa matumizi ya mtandao katika kukusanya habari,
kuziboresha na kuzitumia kwa manufaa ya wananchi.
Ofisa
mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar
na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed,
akitoa baraka zake tayari kuanza mafunzo ya siku tano ya
kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na Tehama mameneja na
waandishi wa habari takribani 60 kutoka redio za jamii mbalimbali
nchini, yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema
Telecentre mkoani Mwanza.
Alisema
kutekelezwa kwa mradi huo ni utekelezaji wa azimio la Windhoek la
mwaka 1991 linalohimiza matumizi ya redio jamii katika kuboresha maisha
ya wananchi kutokana na kuonekana dhahiri kwamba wananchi wanapokuwa na
nafasi ya kujieleza wanaweza kufanya makubwa zaidi.
Akifungua
mafunzo hayo Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii
na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi redio jamii
Micheweni, Ali Mohamed aliwataka mameneja na watendaji wa radio hizo
kutekeleza ushauri wa UNESCO ikiwa na pamoja na kutekeleza maagizo ya
utengenezaji wa vipindi vya vijana ili kupata nafasi ya kushindania
nafasi moja ya upendeleo kwenda Paris , Ufaransa mwakani kwa tamasha la
redio za jamii.
Aidha
aliwataka watendaji kuwa makini katika kazi zao kutokana na serikali
kuweka mazingira sahihi ya uendeshaji wa radio hizo kwa manufaa ya umma.
Mkufunzi
wa darasa la mameneja wa redio mbalimbali za jamii Mkurugenzi Mtendaji
wa ASMET, Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya siku tano ya namna
ya kuingiza kipato pamoja na kutafuta masoko kwa ajili ya kuendeleza
vituo vyao yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yanayoendelea
kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani
Mwanza.
Baadhi
ya mameneja wa redio mbalimbali za jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku
tano ya masoko na ujasiriamali yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na
kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni
(UNESCO).
Meneja wa kituo cha redio Orkonerei FM, Bw. Lucas Kariongi akihoji swali kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo.
Mhasibu
wa kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre, Bw. George
Tumbo akiongaza washiriki wenzake katika kazi za vikundi wakati wa
mafunzo hayo.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akiendesha mafunzo ya matumizi ya Tehama kuwajengea uwezo wa kuweka
kumbukumbu za vipindi na kukusanya vyanzo vya habari kwa kutumia
"Tablet" kwa waandishi wa habari wa redio mbalimbali za jamii
yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa
na shirika la UNESCO yanayoendelea kwenye kituo cha Redio Sengerema
mkoani Mwanza.
Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph
akitoa maelekezo ya matumizi ya "TABLET" katika kuhifadhi na kuandaa
habari kwa kutumia kifaa hicho.
Pichani juu na chini ni washiriki wa mafunzo hayo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya "TABLET".
Chanzo :dewjiblog.com |
Post a Comment