MTANGAZAJI

NAIGERIA:KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO LACHOMWA MOTO NA WANAJESHI WA IMANI YA KIISLAMU

Wanajeshi wa Kiislam wamechoma Kanisa la Waadventista Wa Sabato kaskazini mashariki mwa Nigeria baada ya washiriki wa kanisa hilo 67 kukimbia eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.

Stephen H.Bindas Mwenyekiti wa Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Nigeria yenye makao yake makuu mjini Abuja amesema wanachama wa Boko Haramu wanaotaka kusimika dola ya kiislamu waliteketeza kanisa la Waadventista Wa Sabato la Magar lililoko katika jimbo la Borno sabato ya Agosti 23 mwaka huu.

Magar ni kijiji kilichopo karibu na Maiduguri mjini mkuu wa jimbo la Borno,ambako kuna makanisa saba mahalia yaliyojengwa mwaka 2009 kutokana na msaada wa kifedha toka kwa mpango wa utume wa uinjilisti wa kanisa hilo duniani.

Bindas amesema juma hili kuwa wengi wa waumini hao hawajulikani walipo,baadhi yao wamekimbilia katika jiji la Jos katikati mwa Nigeria na sasa wanaishi kwenye ofisi za makao makuu ya Konferensi ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Bindas ameliambia shirika la habari la Waadventista Wa Sabato Duniani ANN kwa njia ya barua pepe kuwa japo kuwa hakukuwa na vitisho kwa makanisa ya Waadventista ,makanisa mengine ya kikiristo yamekuwa yakikutana na kadhia hiyo,na ametoa wito kwa waumini wote duniani kuombea kanisa nchini Nigeria.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.