MTANGAZAJI

DODOMA:WAZIRI MKUU AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI

Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda amewataka watanzania kudumisha amani,upendo na mshikamano uliodumu kwa miaka 50 ya uhuru hapa nchini.

Akihutubia katika Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma hii leo Waziri Pinda amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuendeleza amani huku akisisitiza kuwa serikali haina dini bali watanzania mmoja mmoja wana dini zao hivyo suala la ubaguzi lisiwepo badala yake umoja katika dini zote udumishwe.

Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja na TBC1 Mheshimiwa Pinda ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania imejenga msingi mzuri wa kutokuwepo kwa migogoro jambo ambalo limeifanya nchi idumu katika hali ya amani na kuliletea taifa la Tanzania heshima kubwa duniani.

Bunge maalum la katiba kupitia kamati ya uandishi imewasilisha jedwali la mapendekezo ya marekebisho ya rasimu mpya ambapo wabunge wanatarajia kupiga kura hii leo katika ibara 289 zilizopendekezwa ili mapendekezo hayo yapitishwe.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.