KAGERA:MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO AJINYONGA
Mwanafunzi
wa Darasa la tano katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihugo Manispaa ya
Bukoba Mkoani Kagera, Ezra Gerald amejinyonga hadi kufa kwa kutumia shuka ya
hospitali, alikokuwa amelazwa kwa kile kinachosemekana alikuwa anasumbuliwa na
homa ya tumbo.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo nakuongeza kuwa mapema juma hili majira
ya asubuhi waliukuta mwalimu wa marehemu
ukiwa kwenye mti nje ya hospitali aliyokuwa amelazwa,huku kukiwa na ujumbe unaonyesha
amechukua uamuzi huo, kutokana na kuchukizwa na uamuzi wa daktari aliyemhudumia
wa kumlaza ili atibiwe ugonjwa ambao hakua anaumwa.
Mkoa
wa Kagera ni miongoni mwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo imekuwa ikihusishwa na matukio
mbalimbali ya kutisha,ambapo Agasti 8 mwaka huu Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni
majambazi walivamia na kuwaua mume na mke na kumjeruhi mtoto mchanga mwenye
umri wa miezi 4 .
Post a Comment