MTANGAZAJI

MARA:WAJAWAZITO 168 WAGUNDULIKA NA MAAMBUKIZI YA VVU JANUARI MPAKA JUNI,2014
Zaidi ya akinamama wajawazito 168 sawa na asilimia 2.9 ya wajawazito 5,755 waliogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika wilaya ya Bunda mkoani Mara wamepatiwa huduma ya kuzuia maambukizi  kutoka kwao kwenda kwa watoto katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Bunda,Vincent Kateire amesema  kuwa watu 3,870 wakiwemo wanawake 2,700 na wanaume 1,160 wanaoishi na virusi vya Ukimwi wilayani humo wamepatiwa dawa za kuvifubaza katika kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu.

Dk.Kateire ameongeza kuwa wanawake wanaonekana kuambukizwa zaidi kuliko wanaume ambapo katika kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu wanawake 498 kati ya watu 844 waliofika kupima afya zao waligundulika kuwa na virusi vya ugonjwa huo huku wanaume wakiwa ni 346 tu.

Pamoja na mikakati mbalimbali ya serikali inayofanya katika kupunguza kasi ya ugonjwa huo,utafiti imebaina kuwa moja ya vichocheo vya ugonjwa huo wilani Bunda ni baadhi ya wanajamii  kushikilia  mila na desturi potofu hasa za kurithi wajane na kutakasa misiba pamoja na kutokuwa waaminifu katika ndoa kwa kua  na michepuko.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.