MTANGAZAJI

MAKAMBI YA MAGOMENI MWEMBECHAI YAFUNGULIWA RASMI JIONI YA LEO

Makambi ya Mtaa wa Magomeni Mwembechai katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato yamefunguliwa hii leo na Mchungaji wa Mtaa huo Mch Jonas Singo ambaye alitoa somo kuhusu unabii.

Blog hii jana na leo mchana imezungumza na Mhutubu Mkuu  Mch Greg Clay Davis akiwa Accra Ghana ambaye ataambatana na mkewe  Chrys Davis amesema atawasili kesho na amefurahi kupokea taarifa ya kuja kuhudumu kwenye kambi hilo baada ya kuhitimisha mkutano wa juma la uamsho katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato huko Kigali.

Wachungaji wengine watakaokuwepo ni Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Kanda ya Mashariki mwa Tanzania (ETC) Mch Mark Walwa Malekana na Mch Oscar Mashishanga.

Fahamu neno kuu la mkutano, tarehe na wahudumu wakuu
Pata utangulizi na ukaribisho maalumu kutoka kwa Mchungaji wa mtaa huu Jonas Safiel Singo
Fahamu wasifu wa wahudumu wa kambi hili kwa juma zima (Picha wa Hisani ya Injili Leo Blog)

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.