MTANGAZAJI

MWANZA:MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA KITAIFA YANAFANYIKA MWANZA



Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Dr Binlith Mahenge leo amefungua maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu mkuu wa mkoa wa mwanza Baraka konisaga amesema maadhimisho hayo yanafanyika kwenye uwanja wa furahisha jijini humo na yatafikia kilele juni 5 mwaka huu , huku wageni kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuudhuria katika maadhimisho hayo.

Konisagi amesema maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ya tunza mazingira ili kukabiliana na tabia nchi, ni kuhimiza juu ya  ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa na changamoto mbalimbali katika taifa

Amesema mabadiliko hayo yatafanyika kwa kufanya usafi, kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira kwa njia  ya makongamano, kupanda miti, kuzoa taka,na kuondoa magugu maji katika ziwa Victoria pamoja na ufugaji wa nyuki.

Naye naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa rais mazingira Angelina Madete amesema mabadiliko ya tabia nchi yamesababishwa na gesi joto ambazo hutokana na shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile viwanda ambazo zimeongezeka kwenye uso wa dunia.

Ameongeza kusema kuwa mabadiliko hayo yameleta athari mbalimbali zikiwemo za kutotabirika kwa majira ya mvua kutishia visiwa kutoweka ikiwa ni pamoja na maeneo ya misitu mikubwa kupungua kutokana na bionuai.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.