MTANGAZAJI

WAZIRI MKUU WA TANZANIA KUKUTANA NA WAKAZI WA SERENGETI WANAOTAKA KUHAMISHISHWA NA TANAPA



Sakata la uhamishwaji wa wakazi wanaoishi katika vijiji vya
Tamau,Nyatwali na Serengeti vya wilayani Bunda ili kupisha upanuzi wahifadhi ya taifa ya Serengeti umeingia katika sura mpya baada yaWaziri Mkuu Mizengo Pinda kutaka kukutana kwanza na wakazi hao kabla ya kulitolea maelekezo yakuumaliza mgogoro huo.

Mamlaka ya hifadhi za taifa(TANAPA) inawataka wakazi hao wanaoishi katika eneo la ghuba ya Speke jirani na ziwa Victoria kuhama ilikuruhusu upanuzi wa eneo la hifadhi hiyo hali itakayowawezesha kunywamaji kwa urahisi kutoka ziwa hilo sambamba na kupata eneo la malishona maficho.

Katika barua yake aliyoisaini yeye mwenyewe ya Mei 12 mwaka huu yenyekumb.na PM/P/1/569/15 aliyomwandikia mkuu wa mkoa wa Mara, Pindaalisema serikali haina budi kutafakari kwa kina namna ya kutatuamgogoro huo ikiwezekana kwa kutumia mfumo wa Wildlife Management Area(WMA).

Kwa mujibu wa Pinda aliyekutana na ujumbe wa wakazi hao Mei 11 mwakahuu idadi ya wakazi hao aliowataja kuwa ni 13,000 wanaoishi katika
kaya 1,390 na ambao haijajulikana mahusiano yao kiuchumi na ziwaVictoria ni kubwa hivyo siyo busara kuwahamisha bila  ya serikali kufanya tafakuri ya kina.

Hata hivyo takwimu hizo zinatofautiana na zile ambazo zimekuwazikitolewa mara kwa mara na serikali wilayani humu zinazoonesha kuwawakazi wanaotakiwa kuhama ni 8,112 na siyo zaidi ya hapo.

Hivyo Pinda ameiagiza wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikianana ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara kumwandalia ziara maalum harakaiwezekanavyo ya kuvitewmbelea vijiji hivyo na kukutana na wakazi haoili aone hali halisi kabla ya kutoa maelekezo ya hatua za kuchukuaakisema hana picha kamili hali ya vijiji hivyo na uhusiano wao na ziwaVictoria.

Ujumbe huo wa watu kumi uliokuwa  ukiongozwa na Mzee Alfred Malagiraulitumwa mahsusi na wakazi hao kwa ajili ya kukutana na mamlaka za juuza serikali ili kuwasilisha kilio chao dhidi ya kile walichokiitauonevu wanaofanyiwa na TANAPA wa kutaka wahame mahala hapo walipoishikwa miaka mingi.

Hatua hiyo ya serikali inakuja siku chache baada ya baraza la madiwaniwa halmashauri ya wilaya hiyo kupinga hoja hiyo ya kuwahamisha wakazihao likiitaka mamlaka husika kuboresha mazingira ya uhifadhi ndani yahifadhi hiyo badala ya kuwahamisha kwa vile wako hapo kwa muda mrefu.


Katika kikao chao  kilichofanyika Mei 7 madiwani hao walisema mbali nasababu hiyo pia kitendo cha kuwahamisha kitawaathiri kiuchumi,kijamiina kisaikolojia kwani walishajiwekeza mahala hapo kwa muda mrefu bilakuwa na wazo lolote la kuhama na kutaka maamuzi mbalimbali ya serikalidhidi ya jambo hilo yazingatiwe.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.