KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MZIZIMA LASAIDIA WATU WASIOJIWEZA
Chama ya kinachowaunganisha wanaume na wanawake wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato AMO DORKAS katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Mzizima jijini Dar es salaam
wametembelea kituo cha watu wasiojiweza cha Nunge kilichoko jijini Dar es
salaam na kutoa misaada ya kijamii na kiroho.
Kituo
hicho ambacho kipo chini ya Serikali
kina idadi ya wazee 37, watoto wanaoishi na ulemavu wa kusikia 23 na
watoto yatima.
Sambamba
na kutoa huduma ya neno la MUNGU pia
wametoa msaada wa mavazi,mchele, sabuni, na unga wa lishe na dawa kwa Wagonjwa.
Kwa
upande wake kiongozi wa mawasiliano wa kanisa la mzizima Kapesa Manyoni ambaye pia alikuwa mkuu wa msafara ameiomba
jamii kuonesha upendo kwa watu wasiojiweza na kwamba wao kama kanisa wataendelea
kufanya hivyo.
Kwa upande wake Afisa Msaidizi wa Kituo
hicho Bwana Mosses Gunza ameshukuru kwa kupokea msaada huo na kusema kuwa ni kuonesha upendo
wa Mungu kwa watu wasiojiweza kwani Hawakupenda kuwa hivyo.
Wazee
hao pamoja na watoto yatima wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwahisha misaada ili iweze kuwafikia kwa
wakati hali ambayo itasaidia upatikanaji
wa mahitaji kwa urahisi.
Post a Comment