MTANGAZAJI

UHARIBU WA MAZINGIRA HUENDA UKAKOSESHA MAJI WAKAZI MJI WA MTWARA



Wakazi wa mji wa mtwara wako hatarini kukosa  huduma ya maji baada ya watu wasiofahamika kuvamia na kuchimba mchanga kwenye chanzo cha maji katika kijiji cha Namayanga kata ya ziwani .

Taarifa zinasema kuwa kutokana na shughuli hizo za uchimbaji mchanga kushamiri maji yamehama kwenye mkondo wake khali inayopelekea wakazi wa maeneo hayo kukosa huduma hiyo muhimu.

Aidha kutokana na na uharibifu huo kumelazimu Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile kupiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika eneo hilo

Asilimia 99  ya wakazi wa Mtwara wanategemea kupata maji kutoka katika vyanzo hivyo na iwapo wachimbaji wataendelea na zoezi hilo basi biashara hiyo itasababisha shida kubwa ya upatikanajji wa  maji katika maeneo hayo.

Akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Mtwara (MTUWASA)Ndugu Kubiri Masunga amesema uharibifu  huo ulianza siku nyingi na kwamba pamoja na hatua kadhaa kuchukuliwa ili kuzuia uhalibifu huo lakini  bado watu wamekuwa wakiendelea na uchimbaji huo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.