UHAMIAJI:WAHAMIAJI HARAMU 400 WALIKAMATWA NGARA JANUARI HADI APRIL 2014
Wahamiaji haramu wapatao 400 raia wa Burundi wamekamatwa na
idara ya uhamiaji wilayani Ngara mkoani
Kagera kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria na kurejeshwa makwao
katika Kipindi maalum cha oparesheni kimbunga iliyofanyika katika mikoa ya
kanda ya Ziwa Victoria.
Ofisa wa idara ya uhamiaji wilayani ngara ndugu Marwa
Kitang’ita amesema wahamiaji hao walikamatwa katika msako maalum kwenye vijiji
vya tarafa ya Rulenge,Kanazi na Nyamiaga
kuanzia January hadi april mwaka huu
Kitang’ita amesema wananchi wa vijiji vya vilivyoko mpakani mwa
nchi jirani za Rwanda na Burundi wanachangia kwa kiasi kikubwa kuwakaribisha
wahamiaji hao na kuwafanyia shughuli mbalimbali ikiwemo kuwachungia mifugo.
Amesema katika msako huo bado viongozi wa vitongoji na
vijiji hawatoi ushirikiano wa dhati ili kuwabaini wahamiaji badala yake
wamekuwa wakilalamikia wanapoutana na
uhalifu hasa wanapoibiwa mali zao.
Pamoja na oparesheni kimbunga kufanyika katika mikoa ya
geita Kagera na kigoma bado wahamiaji wanarejea kwa kisingizio cha kuendeleza
mashamba waliopewa ama kununua kutoka kwa watanzania .
Kitang’ita ameongeza kuwa changamoto kubwa inayokabili idara
ya uhamiaji Ngara ni ukosefu wa vitendea kazi hasa magari na mafuta ya vyombo
vya usafiri na hivyo kusababisha baadhi ya maeneo yaliyoko mbali kutofikika kwa
haraka . wanaoingia katika madaftari ya mabalozi na wenyeviti ili kukabailiana
na wimbi hilo la wahamiaji haramu.
Mkuu wa wilaya ya ngara Costantine kanyasu amewataka
viongozi wa vijiji na mitaa kuorodhesha wageni wanaoingia katika madaftari ya
mabalozi na wenyeviti ili kukabailiana na tatizo hilo
Post a Comment