CAG ASEMA PRIDE TANZANIA SI MALI YA SERIKALI
Taasisi ya Pride Tanzania ambayo hutoa mikopo midogo midogo
kwa wajasiriamali imetoweka kwenye
orodha ya mali zinazomilikiwa na serikali.
Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Inasema taasisi hiyo
ilianzishwa mei mwaka 1993 chini ya sheria ya mahakama.
Amesema dhumuni la kuanzishwa taasisi hiyo ni kutoa mikopo
midogo midogo kwa wajasriamali nchini.
CAG amesema taarifa
za msajili wa hazina inaonesha kuwa uwekezaji wa serikali katika kampuni
kufikia juni 30 mwaka 2008 hisa zote za Pride zinamilikiwa na serikali .
Taarifa hiyo inasema mtaji hadi juni 30 mwaka 2008 unaonesha kuwa ni Shilingi za
kitanzania 2.301 bilioni ,na fedha za wanahisa wengine zilikuwa ni jumla ya shilingi 2.198 bilioni,
na hivyo kuufanya mtaji mzima kuwa shilingi 4.499 bilioni.
Kwa mujibu wa taarifa ya masajili wa hazina iliyoishia juni
30 mwaka jana shirika hilo halipo tena kwenye moja ya mashirika ya umma.
Hata hivyo amesema kuwa uhalali na sababu za kuondolewa kwa
shirika hilo katika orodha ya msajili wa
kampuni hazikufahamika.
Kwa mujibu wa sheria
ya ukaguzi wa umma namba 11 ya mwaka 2008 kila shirika la umma linatakiwa
kupeleka hesabu kwa CAG Kukaguliwa katika kipindi cha miezi 3 baada ya mwaka wa
fedha kukamilika .
Hata hivyo hesabu za pride Tanzania hazijawahi kuwasilishwa
kwa CAG kama inavyotakiwa kisheria jambo linaloibua maswali kwa jamii.
Post a Comment