TABORA:JESHI LA POLISI LAKAMATA WANNE KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA SIRAHA NA SARE ZA JESHI
Jeshi la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu
wanane kwa tuhuma za makosa mbalimbali,ikiwamo ya umiliki wa silaha kinyume cha
sheria na kukutwa na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kamanda wa polisi mkoani Tabora Susan Kaganda
amesema kuwa matukio hayo yametokea maeneo tofauti na watuhumiwa wamekamatwa
kwenye operesheni ya kukabiliana na uhalifu.
Kaganda amedai kuwa katika tukio la kwanza la
kukamatwa mkazi wa Inyonga akiwa na Risasi 307 za Bunduki aina ya SMG,mtuhumiwa
alikiri kujihusisha na uchuuzi wa risasi na matukio mbalimbali ya unyang`anyi
wa kutumia silaha .
Jeshi la polisi nchini Tanzania linatoa wito kwa raia wote kushirikiana na jeshi
hilo ikiwemo kutoa taarifa za kuwabaini wahalifu katika lengo la kukomesha vitendo
vya kihalifu nchini humo.
Post a Comment