MTANGAZAJI

AFUNGWA MIAKA MITANO BAADA YA KUKIRI KUMWIBIA NG'OMBE WATANO BABA YAKE MZAZI.Mahakama ya wilaya ya Bunda mkoani Mara  imemhukumu Magembe
Buka(23) mkazi wa kijiji cha Sarama Kati cha wilayani humo kwenda
kutumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukiri kumwibia baba
yake mzazi ng’ombe watano wenye thamani ya sh.1.2 milioni.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwendesha mashtaka mkaguzi msaidiziwa polisi Masoud Mohamed aliiambia mahakama hiyo kuwa Magembe ambayeni mtoto wa kuzaliwa wa mzee Buka Mange (63) mkazi wa kijiji hicho alitenda kosa hilo Mei 10 mwaka huu.

Masoud amesema siku hiyo mshtakiwa aliwaiba ng’ombe hao na kuwakabidhi kwa rafiki yake ambaye hata hivyo hakumtaja jina aliyekamatwa nao akiwa katika harakati za kuwatafutia soko huku yeye akifanikiwa kutorokea kusikojulikana kujiepusha na mkono wa dola.

Baada ya maelezo hayo Magembe ambaye muda wote alikuwa akisikiliza kwa makini huku  alikiri kufanya kosa hilo hali iliyomfanya mwendesha mashtaka aiombe mahakama hiyo kumpa adhabu kali ili liwe fundisho kwa wengine.

Kwa mujibu wa Masoud vitendo vya wizi wa mifugo vimekithiri sana
maeneo mbalimbali nchini ukiwamo mkoa wa Mara hata kuvuruga hali yaamani na utulivu ndani ya jamii hivyo hapana budi kwa vyombo vya
kisheria kutoa adhabu kali kwa wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Akitoa hukumu hiyo hakimu Ahmad Kasonso amesema mahakama imefurahishwana ushirikiano aliouonesha mshtakiwa ambaye amekiri kosa lake inampa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwa wengine.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.