MTANGAZAJI

WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA WATAKIWA KURIPOTI UTALII

Serikali ya Tanzania imevitaka vyombo vya habari kutumia ushawishi kwa jamii kwa kuripoti shughuli za utalii na kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini humo kuhamasisha utalii wa ndani na nje.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania Maimuna Tarshi akifungua warsha jana ya wahariri wa vyombo vya habari  inayoendelea jijini Mwanza amesema ni wakati muafaka kwa vyombo vya habari kuamua kwa makusudi kuongeza uhamasishaji kwa jamii iweze kuvitembelea vivutio hivyo.

Maimuna amesema kuwa utalii ni moja ya sekta ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Tanzania ambapo kwa mwaka jana inakadiriwa uliingiza dola za kimarekani bilioni 1.8

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.