HAKIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI NA TAKUKURU KWA MADAI YA KUJIPATIA FEDHA KWA KUBAMBIKIA KESI
Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Bunda juzi imemfikisha
katika mahakama ya wilaya hiyo,hakimu wa mahakama ya mwanzo ya Kenkombyo ya
wilayani humo Emanuel Paul Mng’ware (32) akidaiwa kutoa hati za mashtaka hewa
kwa watu wasio na hatia ili ajipatie fedha.
Taasisi hiyo pia inamtafuta ofisa mtendaji wa kijiji cha Kibara A,BerthaWitness Lameck (38) ili afikishwe mahakamani kwa madai ya kutumiwa na hakimu huyo kusambaza hati hizo kwa walengwa waliokuwa wakiwatoza faini kati ya sh.60,000 na 150,000 kwa makosa ya kubambikiwa.
Mwanasheria wa TAKUKURU, Eric Kiwia amedai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wamechezesha mchezo huo kwa muda mrefu kwa watu mbalimbali kabla ya taasisi hiyo kubaini na kuweka mtego kwa watu watano kati ya Aprili 22 na 23 uliofanikisha kuwakamata.
Amesema pindi washtakiwa walipokuwa wakiwakamata wananchi hao wasio na hatia ambao wengi wao ni wavuvi na kuwafikisha mahakamani waliwabambikia kesi ya uvuvi haramu wakiwataka walipe kiasi hicho cha fedha ili kujinusuru na kifungo cha miezi sita jela walichokuwa wakitishiwa kupewa.
Amesema uchunguzi wa awali uliofanywa na tasisi hiyo umebaini kuwa
hati hizo zilizokuwa zitolewa na hakimu huyo zilikuwa ni karatasi
zilizoiandikwa kwa mkono tena kwenye kipande cha karatasi bila mhuri
wowote wa mahakama huku fedha zilizokuwa zikitozwa kama faini zikiwa hazikatiwi risti.

Hakimu Ahmad Kasonso anayeisikiliza kesi hiyo ameiahirisha hadi Juni
16 mwaka huu huku akitoa hati ya kukamatwa mara moja kwa ofisa
mtendaji huyo ili afikishwe mahakamani hapo kujibu mashtaka yake
ambapo Emanuel Paul yuko nje kwa dhamana.
Post a Comment