MTANGAZAJI

TABORA: SABA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA ASKARI POLISI


Jeshi la Polisi mkoani Tabora limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 7 waliohusika katika tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha na mauaji ya askari polisi wawili lililotokea Aprili 28 mwaka huu  katika tarafa ya Ussoke wilaya ya Kaliua mkoani humo.

Akitoa taarifa kwa waandishi waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Suzan Kaganda amesema askari waliouawa walikuwa katika kutekeleza majukumu yao huko Ussoke wilayani Kaliua ambapo aliwataja kuwa ni F.5179 Pc Jumanne na G.3388 Pc Shaaban.

Amewataja waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo kuwa ni Silvester Mussa maarufu Kingwendu (31) mkazi wa Mkuyuni Tambukareli Mwanza,Sadiki Hamis Rushikamwa au Sadiki Milambo maarufu  White (28) mkazi wa mihogoni Tabora na Abel Benedicto ambaye pia huitwa Mwendo wa saa (23) mkazi wa Muungano wilaya ya Urambo.

Wengine waliokamatwa ni Francis Kashinje ama Masanja (38)mkazi wa Nansio Ukerewe, Haji Athanas Simba (50) mkazi wa Ussoke,Mussa Khatibu Ally ama Mussa Bonge (49)  mfanyabiashara wa nafaka ambaye ni mkazi wa Mwanza road na Ramadhan Kasimu Mkunya maarufu  Rama Manywele au Rama Mrefu mkazi wa Tabora.


Kamanda amebainisha kuwa baada ya mahojiano watuhumiwa hao walikiri kushiriki matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo la mauaji ya askari polisi wawili  na baada ya upekuzi walikutwa na silaha aina ya Pistol Glock 17 yenye namba za usajili TZ Car 91968 ikiwa na magazini yenye risasi 5.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.