MTANGAZAJI

PROFESA MUHONGO AIOMBA SERIKALI KURUDISHA ADHABU YA VIBOKO SHULENI

Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameiambia serikali kurudisha viboko mashuleni ili kurejesha nidhamu kwa wanafunzi mashuleni na kuinua kiwango cha elimu kinachoshuka nchini siku hadi siku.

Mhongo ameyasema hayo katika ziara yake mkoani mara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini REA, wakati akiwa katika Kijiji cha Magoto kata ya Ganyange Wilayani Tarime.


Mkoa wa Mara ulifanya vibaya katika matokeo ya kidato cha nne na darasa la saba mwaka jana, matokeo ambayo yaliufanya mkoa huo kuwa wa 22 kati ya mikoa 26 ya kitaifa.


Sababu zinazofanya kushuka kwa elimu shuleni hapo ni pamoja na utoro wa wanafunzi, ambapo walimu wa shule hiyo wanagopa kuwafuatilia wanafunzi hao kwa kuwa na mahusiano mabaya na wazazi.


Profesa Muhongo amesema jamii haina budi kuachana na tamaduni zilizopitwa na wakati kama vile ukeketaji na tohara, kuozeshwa kwa binti ama vijana wa kiume wakingali wadogo kunachangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika mkoa huo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.