MTANGAZAJI

IDADI YA WALIOKUFA KUTOKANA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM YAFIKIA 41


Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita imefikia 41.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki amesema vifo 25 vimethibitishwa na amewaagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu wengine ambao hadi sasa hawajaonekana waliko.


Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa eneo la Ilala vilitokea vifo 11 ingawa inahisiwa kuwa watu wawili hawajaonekana.


Kinondoni vifo ni saba huku wengine 11 wakidaiwa kuzikwa bila jeshi la polisi kupata taarifa yoyote na temeke vifo ni saba.


Sadiki ametaka uchunguzi wa polisi ufanyike kwa kila familia zilizokubwa na msiba hususani Kinondoni kuthibitisha kama vifo hivyo 14 vilitokana na mafuriko.
No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.