MTANGAZAJI

HALMASHAURI ZA WILAYA NA HIFADHI ZA TAIFA ZATAKIWA KUWA NA MATUMIZI BORA YA ARDHI

Hifadhi za Taifa na halmashauri za wilaya zinazozunguka maeneo nyanda za juu kusini mwa Tanzania zimetakiwa kuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi.

Katika kuhakikisha lengo hilo linafikiwa, mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST) umeanza kutoa mafunzo hayo kwa watendaji wa halmashauri zinazozunguka hifadhi za kusini.


Mratibu wa SPANEST, Godwell Meing’ataki amesema mafunzo hayo ya siku tano yanahusisha watendaji kutoka halmashauri za wilaya ya Mbeya, Wanging’ombe, Makete, Chamwino, Katavi na Iringa.


Meing’ataki amesema halmashauri zinazozunguka hifadhi za Taifa zinatakiwa kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi ili kuepukana na migogoro inayopelekea baadhi ya wananchi wake kuvamia kwa matumizi yao maeneo mbalimbali yaliyohifadhiwa.


Meing’ataki amesema ardhi ni rasilimali ya msingi; ili kukidhi mahitaji yake hapana budi watumiaji wake wawe na utaratibu na mipango itakayoathiri wengine.


Amesema Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ni utaratibu wa kutathimini na kupendekeza namna mbalimbali za uhifadhi na matumizi ya maliasili au rasilimali ili kuinua uchumi wa Taifa na kuondoa umasikini.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.