MTANGAZAJI

TFDA WAOMBA WANANCHI KUWAPA TAARIFA ZA BIDHAA FEKI


 
Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA)Kanda ya Ziwa Victoria ,imewataka wananchi kuipa taarifa pindi wanaponunua bidhaa feki,zilizomalizika muda wake na ambazo hazijasajiliwa.

Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa,Moses Mbambe,amesema hii leo jijini Mwanza kuwa wananchi wanapaswa kuisaidia Mamlaka hiyo katika kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu,ambao wamekuwa wakiingiza nchini bidhaa bandia, zilizochini ya viwango vya ubora,na hata zisizo na usajili.


Moses Mbambe amesema, bidhaa nyingi feki, na hata zile zilizopigwa marufuku hapa nchini hupitia Ziwa Victoria kwa njia ya mitumbwi,na madhara yake sasa ni makubwa kwa jamii, ambayo haina budi kutoa taarifa mara wanaponunua bidhaa zenye madhara na zinazotia mashaka.


Miongoni mwa bidhaa zilizopigwa marufuku na serikali ni pamoja na zile za kuongeza makalio ya akina mama na zile za kujichubua ambazo zimethibitika kuwa na madhara ya kiafya.


Na:Conges Mramba-Mwanza

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.