MTANGAZAJI

MTANGAZAJI WA BBC KOMLA DUMOR AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 41


Komla Dumor presenting Focus on Africa 17/01/2014
Picha  ya Komla Dumor akitangaza kipindi cha Televisheni cha  Focus on Africa ya BBC-Janury  17,2014 (Chanzo:BBC)

 Mtangazaji wa BBC Komla Dumor mzaliwa wa Ghana amefariki  dunia  Januari 18,2014 nchini Uingereza.

Tovuti ya BBC imeeleza kuwa  mtangazaji huyo aliyezaliwa mwaka 1972 amefariki ghafla nyumbani kwake London,Uingereza .

Komla Dumor  ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kutangaza kipindi cha BBC cha  Focus on Africa ambacho hapa Tanzania huwa  kinaonekana kupitia Star TV kwa lugha ya kiingereza alionekana akitangaza kipindi hicho siku ya ijumaa Januari 17,2014.

Mtangazaji huyo ambaye kabla ya kujiunga na katika matangazo ya radio ya BBC mwaka 2007  alikuwa ni mwandishi wa habari alifanyakazi nchini Ghana ambapo mwaka 2003 alipata tuzo ya mwandishi bora wa mwaka nchini humo ambako alikuwa akitangaza kipindi cha asubuhi cha Joy FM kwa muda wa miaka 10.


Mwaka 2009 Komla Dumor alikuwa alipata nafasi kuwa mtangazaji wa kwanza kutangaza habari za biashara za Afrika katika BBC dira ya dunia idhaa ya kiingereza.

Watu mbalimbali wanaomfahamu mtangazaji huyo, kupitia mitandao ya kijamii wameonekana kushtushwa na habari za kifo chacke.

 Tovuti ya myjoyonline.com inayoandika habari za Ghana imeandika kuwa Komla Dumor alikuwa ni mtangazaji wa habari pekee wa BBC toka Afrika Magharibi hadi mauti yalipomkuta.

Tovuti hiyo inaeleza kuwa Dumor aliingia katika uandishi wa habari japo hakusomea uandishi wa habari bali alianza kusoma udaktari lakini alibadilisha  na kupata shahada ya sayansi ya jamii na saikolojia katika Chuo Kikuu cha Ghana na akasoma shahada ya uzamili ya uongozi ya Chuo Kikuu cha Harvard.

Alioana na Kwansema Dumor na walibahatika kupata watoto watatu  
  

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.