MTANGAZAJI

JAJI NCHINI INDIA ASEMA KUFANYA NGONO KABLA YA NDOA NI UKIUKAJI WA MAADILI

Jaji mmoja nchini India amesema kuwa kufanya ngono kabla ya ndoa ni jambo linalokiuka maadili na linalokwenda kinyume na kanuni za dini.

Jaji Virender Bhat alitoa matamshi hayo baada ya kutoa uamuzi kuwa watu wawili wanaokubaliana kufanya ngono kwa ahadi ya kuoana , sio ubakaji.
Ngono kabla ya ndoa nchini India ni jambo linaloonekana kama mwiiko katika jamii nyingi nchini humo.

Mwaka jana, mahakama mjini Delhi ilisema kuwa uhusiano wa watu wawili wanaosihi pamoja bila ya ndoa ni jambo linalokiuka maadili na kusema kuwa hiyo ni tabia ya watu wa nchi za magharibi.

Jaji Bhat husimamia mahakama moja nchini India ambayo huharakisha kesi zinazohusiana na dhuluma za kingono dhidi ya wanawake.

Alitoa matamshi yake alipokuwa anamwondolea kosa la ubakaji mwanamume mmoja aliyekua ameshitakiwa kwa kosa hilo.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29, alikamatwa baada ya mwanamke anayefanya kazi katika kampuni moja kulalamika kuwa mwanamume huyo alimbaka mwaka 2011.
Mwanamke huyo alilalamika kuwa mwanamume huyo alifanya naye ngono baada ya kumuahidi kuwa angemuoa jambo ambalo halikufanyika.

Jaji alisema kuwa uhusiano wao wa kingono ulitokana na ahadi kuwa mwanamume angemuoa lakini hakumbaka na wala kitendo chake sio ubakaji.

"wakati mwanamke aliyekomaa anapokubali kufanya ngono na mwaname kwa kuwa amemuahidi kuwa atamuoa , hakuna wa kulaumu hapo kwani mwanamke anapaswa kujua ikiwa mwanamume huyo hatatimiza ahadi yake, yeye ndiye anapata hasara,'' alisema jaji Bhat

Mnamo mwaka 2010, mahakama ya juu zaidi ilitupilia mbali kesi dhidi ya mwanamke muigizaji aliyeunga mkono haki ya wanawake kufanya ngono kabla ya kuolewa. Mahakama pia iliidhinisha mwanamke na mwanamume kuishi pamoja bila ya kuoana.
Chanzo:BBC

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.