AJAAT YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI KUHUSU HARAKATI ZA KUJILINDA DHIDI YA VVU NA ATHARI ZA UKIMWI
Mratibu wa UNAIDS nchini Tanzania Dr Patrick Brenny akifungua mafunzo |
Chama Cha Waandishi wa Habari Dhidi ya UKIMWI Tanzania (AJAAT) kimefanya
mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari Dar es salaam
.
Mafunzo hayo yaliyodhaminiwa na Shirika la Kimataifa Kuhusu Masuala ya
UKIMWI la UNAIDS Tawi la Tanzania
(UNAIDS-Tanzania) yanalenga kuwaelimisha waandishi wa habari mbinu bora za jinsi ya
kupiga vita Unyanyapaa na Ubaguzi unaohusiana na VVU/UKIMWI kwa kutumia taaluma
yao.
Aidha mafunzo haya pia yatatoa mwanya wa kufanya tathmini ya mchango wa
vyombo vya habari katika harakati za kutokomeza maambukizi ya VVU na katika
kupambana na athari za UKIMWI, kubadilishana mawazo na uzoefu na wadau walio
katika harakati hizo na kuweka mikakati ya pamoja katika kufanikisha azma hiyo.
Post a Comment