TAMKO LA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO KUHUSU TIBA MBADALA
KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO – TANZANIA UNION MISSION
Mkutano wa Mwisho wa Mwaka
Mkutano wa Mwisho wa Mwaka
Uliofanyika tarehe 21 na 22 Novemba, 2012
MSISITIZO WA TAMKO KUHUSU HUDUMA ZA AFYA LA KANISA LA WAADVETISTA WA SABATO LILILOPITISHWA MWAKA 2009, Silver spring, Maryland, USA
Kwa kuwa Kanisa la Waadventista wa Sabato limejitoa kwa dhati kuzingatia ukweli, haki, uhuru, busara, na usahihi katika uendeshaji wa mipango yake yote,Na Kwa kuwa utoaji wa huduma za afya unapaswa kuaminiwa na umma kwa kutokuingiza mgongano wa maslahi binafsi na majukumu ya kitaalam,Na kwa kuwa kuna watu walioanzisha huduma za kile kinachoitwa mfumo wa Tiba Mbadala ambao hauendani na ujumbe wa afya wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Na kwa kuwa Kanisa la Waadventista wa Sabato halina kile kinachoitwa Tiba Mbadala, vyuo vya tiba mbadala, wataalam wa tiba mbadala na mfumo wa tiba mbadala kama ambavyo imekuwa ikitumiwa na wale wanaodai kutumia mfumo huo wa tiba kwa kunukuu maandiko ya Ellen G. White huku wakiwakatisha tamaa watu kwenda hospitali isipokuwa kwenye vituo walivyoanzisha kama sanitariam.
IMEPITISHWA: Kusisitiza tamko lililopitishwa katika baraza la mwisho wa mwaka 2009 la Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato kule Silver Spring, Maryland, USA linasomeka hivi:
“Kanisa la Waadventista wa Sabato linatamka kwa dhati sharti na shabaha ya Huduma ya Afya inayolenga katika kufanikisha ustawi wa washiriki wake na jumuia inayohudumiwa, na kuboresha afya duniani kwa ujumla.
Kanisa la Waadventista wa Sabato - Makao Makuu - linarudia tena kutoa ahadi yake kwa kanuni ya hadhi ya utu na usawa, haki ya jamii, uhuru, kujitawala, uwezekano wa kupata chakula na maji safi, na uwezekano wa kila mtu kuifikia huduma ya afya iliyopo bila ubaguzi. Kupitia huduma yake ya kuhubiri, kufundisha, kuponya na kuwafanya watu kuwa wanafunzi (discipling).
Kanisa linatafuta kuwakilisha utume wa Yesu Kristo kwa namna itakayowafanya waonekane: Kuheshimika ulimwenguni kama wanaofundisha mfano wa ushuhuda timilifu (evidence based) uliojengeka katika kuishi kwa kufuata kanuni za afya katika huduma ya afya ya msingi.
Kuonekana wanaaminika wakati wote, huku wakihusiana na mashirika mengine kwa namna ya uwazi wakiwa na malengo na maono yenye ulinganifu katika jitihada za kupunguza maumivu na kushughulikia afya ya msingi na ustawi. Kutambuliwa kwa upeo wake usio na masharti wa kuwakubali wote wanaotafuta afya hii ya msingi na ustawi. Kuhusika sio tu kiutawala, bali pia kiutendaji katika ngazi zote pamoja na kila kusanyiko na washiriki wa Kanisa katika huduma hii ya Afya na Uponyaji.
Na Ieleweke pia kuwa, wale wote wanaojishughulisha na Tiba Mbadala hawawakilishi filosofia ya Kanisa la Waadventista wa Sabato kuhusu Huduma ya Afya isipokuwa wanafanya hivyo kwa manufaa yao wenyewe.
Maoni ya mtoa taarifa: Nyongeza ya “Kuwafanya Wanafunzi (discipling)” inaweza
kueleweka vizuri katika kazi ya afya kama Kunasihi (mentoring)
Imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania
Dr Livingstone Kingu
Post a Comment