MTANGAZAJI

RAIS WA ZANZIBAR AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALIMBALI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali M.
Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbali mbali za
Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na

Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee Dkt Shein kwa
mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50 (4) cha katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984, Rais amemteuwa Mdungi Makame Mdungi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar.

Aidha Dkt. Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 61

(2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 amemteuwa Khamis Jabir Makame
kuwa Mkuu wa Wilaya Kaskazini B Unguja.Uteuzi huo unaanza leo tarehe
16 Mei 2012,

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.