MTANGAZAJI

VITU VINAVYOFANYA ADUI UJINGA KUWATAWALA WATANZANIA WENGI

1.Kazi za magazeti ya udaku na mengine yasiyokuwa makini,Haya ni
chanzo kikubwa kwa asilimia 80% ya watanzania wanayoyatumia  hivyo
kuishia kupanda mbegu ya ujinga na hivyo kupelekea kila wiki kuvuna
wajinga  wengi sana ,pia haya magazeti mengine ambayo yana andika wazo/
hisia  za mwandishi kuwa  ndio tukio  na hali halisi(facts) nakuwa
ndio ndoo kichwa cha habari siku hiyo na kuishia kuvuna  watu
wanajiendesha kutokana na wazo la mtu(mwandishi) badala lake
mwenyewe.athari yake ya kazi  ya haya magazeti ni  kuwa na   watu
wasikuwa wakuweza kuchangia mada au ajenda kwa kuwa wana taarifaa za
watu sio walizojaza kichwani na sio mada/ajenda hivyo ukiwaleta katika
mada ni weupe.

2.Exposure(kutoka nje ya nchi),nchi yetu ni ya uchumi huru lakini watu
kiukweli bado tupo tuna fanya  na kuishi maisha ya uchumi usio
huru(closed economy) watanzania karibia wote waliotoka nje ndio ambao
wanaojua mambo na ndoo inasemekana ndoo wenye ushindani katika soko la
dunia lakiniasilimi yao ni ndogo sana ,kama ndoo hivi tunahitaji
tujiulize je kama tunataka kuendelea wakati wanafunzi wanaofanya
exchangeprogramnje ya nchi ni wachache,wanaoenda kusoma ni
wachache,kufanya kazi bado ni wachache je tutawezaje kuendele kutoka
hapa tulipo?muda sasa umefika kuanza kupeleka ndugu zetu nje ya nchi
kwa wingi wakaitangaze  na kuleta teknolojia mpya na mawazo tofauti
nakusababisha kuwa na taifa la wajanja,inasemekana nchini Nigeria
karibia kila mnaigeria ni mjanja hakuna wa kumdanganya.

3.Kutokuwa na muda wakufikiri angalau nusu saa kwa siku,Tanzania
maeneo ya wazi kwa umma ya kumpuzika  ni madogo na machache sana mjini
jua kali wiki nzima watu wapo resi n a maisha yao  litakalo tokea
kesho au baadae na liwe,watu wengi ni waathirika wa brain drain,muda
wa kufikiri hakuna na kama kam hujafikiril eo kesho kuna mtu
atakufikiria na kukutawala .Sasa nini tufanye kwa hili tutenge maeneo
mengi ya wazi kwa mapauziko kwa watanzania,elimu kupitia media juu ya
umuhimu wa kufikiri tukumbuke kama hatufirii leo kesho mtu atafikiria
na kukutawala.

4.Kusoma vitabu,kuna msemo wa siku nyingi unasema kama unataka
kumficha mwafrika basi weka ujumbe kwenye kitabu,mara zote kama
uantaka ukombozi wa kimaarifa basi huna budi kujifunza kutoka kwa
wengine na wewe pia ujue nini ufanye ili ulete mabadiliko tofauti,kuna
aina tofauti za vitabu kwa watu wa dini vitabu vyao vitakatifu bado
hata theluthi hawafikia walio wengi,muda sasa umefika acha kupenda
kusikiliza anzan sasa kusoma mwenye ili uwe huru,nunua vitabu kuna vya
kukusaidia wewe ufanikiwe kifedha,furaha,siasa,historia za mashujaa
mbalimbali,mara ya kwanza utaona kawaida lakini kadri unavyozidi
kuendelea kusoma vitabu ndoo yanakuwa maisha yako  ya kila siku na
kuwa sawa na kuamka mara ya pili.

5.Mfumo wa elimu na sera ,mfumo wetu  unahitaji mabadiliko sana katika
hii dunia ya utandawazi,ndio kuna dunia ziliendelea kwa lugha zao
lakini mimi sina maana tukitupe Kiswahili bali ni kama tuna cheza
mchezo wa makusudi wa kutengeneza matabaka  katika jamii,mfumo
unahitaji kubadilika  mfano masomo yote yanatakiwa kufundishwa kwa
kiingiingereza kuanzia chekechea,primary na kuendelea, huwezi
kumfundisha mtu kiingereza na wote wakajua kiingereza wakati umri wa
wao (kipindi mtoto ubongo wake una elewa zaidi sana umepita yaani
kakomaa tayari)ni sawa na mafunzo ya sarakasi kama hukufanya ukiwa
mdogo viungo bado havijakomaa  ukija ukubwani kama ukifanikiwa itakuwa
kwa shida sana na dunia kuanzia china ,japan ,urusi,kote huku sasa
watu wanaongea kiingereza,tuanze sasa kujifunza English  maaana mambo
mengi yameandikwa kwa kiingereza.Wazazi tafuteni shule za English
medium wakasome maana taifa la kesho kama hamjafanya hivyo watoto wenu
watatupwa nje ya mfumo msifurahie shule za kata ni mtego wa
kutengeneza tabaka la tatu kubwa.

6.Meditation,meditation ni muhimu sana kwa taifa kama hili,kwa
maendele yaliyo bora na kuwa huru meditation inahitajika,mara nyingi
tunapata stress tutokapo makazini,miangaikoni,tuna hitaji meditation
ili kuondokana na haya yote,pia kuirefresh akili zetu zianze upya.kuwa
na fikra sahihi

7.Kazi inayofanywa  na television na redio station,maisha ya siku hizi
taarifa ndio ufunguo wa maisha na sio tena elimu ya darasani(formal
education) japo kuwa inaumuhimu pia,television  na redio station
zinafanya kazi ya  kusambaza hizi taarifa kwa asilimia kubwa ya
watanzania,lakini sio taarifa za kufanya wao wawe bora na wajanja sana
katika hiii dunia,kuna siku nilibahatika kutizama  kituo kimoja cha
television mtangazaji aliyekuwepo pale yaani wewe ndoo unatakiwa
umuambie au ndoo umpe data  ilikuwa inatia huzuni kwa mtu kupewa
mamlaka ya kutangaza halafu hakuna kitu kichwani alichofanya juhudi
aweke ili awaaambie watu,tunahitaji kufanya mabadiliko katika vyombo
vetu vya habari kuzifanya taarifa za kuwaza kijanja na kisasa na
kujenga mtu.

Imeandaliwa na :
Deogratius Kilawe:
Achivers Club-President
Chairman Afri Youth Organization
0717 109 362                                       
Mfanyabiashara hapa Daresalaam

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.