MTANGAZAJI

MGOMO WA MADAKTARI TANZANIA:MIZENGO PINDA KUKUTANA NA MADAKTARI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo (Jumapili, Januari 29, 2012) atakutana
na madaktari waliofanya mgomo kwenye ukumbi wa Karimjee kuanzia saa
4:00 asubuhi.

Madaktari hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wanaomba kuonana na Waziri

Mkuu na mara zote Waziri Mkuu amekubali kuonana nao lakini
hawakutokea. Pamoja na kukubali huko kwa Waziri Mkuu, tarehe 25
Januari 2012 katika Mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari
aliwaomba Madaktari kuwa alikuwa tayari kuonana nao lakini
hawakutokea.

Ili kuendeleza jitihada za kutaka kuonana na madaktari hao, Waziri

Mkuu alituma Uongozi wa Serikali ukiongozwa na Mawaziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii; na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
kuonana na Madaktari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight tarehe 27
Januari 2012. Kwenye Mkutano huo madaktari waliwasilisha malalamiko
yao na kuomba kuonana na Waziri Mkuu. Kufuatia maombi hayo, Waziri
Mkuu amewaandikia madaktari hao barua ya kuwataka kuonana nao Kesho,
tarehe 29 Januari 2012 kwenye Ukumbi wa Karimjee, saa 4:00 asubuhi.

Kabla ya kufikia uamuzi huo, kulikuwa na mawasiliano kati ya Ofisi ya

Waziri Mkuu na Uongozi wa Medical Association of Tanzania (MAT) na
baadaye Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Madaktari kuhusu mgomo wa
Madaktari unaoendelea.

Aidha, Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefanya mazungumzo na

Wawakilishi wa Madaktari na Madaktari wenyewe kwenye Ukumbi wa Hoteli
ya Starlight ili kuweza kupata ufumbuzi wa matatizo yaliyowasilishwa
Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anawasihi Madaktari wote kuhudhuria mkutano.IMETOLEWA NA:

OFISI YAWAZIRI MKUU
DAR ES SALAAM
Na:Yona Maro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.