MTANGAZAJI

MASKINI NCHINI TANZANIA WANA WASIWASI NA ELIMU YA WATOTO WAO

Utafiti wa kila mwezi unaofanywa na Twaweza ikishirikiana na World Bank--Dar es Salaam Mobile Survey--unaonesha kuwa wazazi wenye uwezo kifedha wanaridhika na elimu wanayopata watoto wao, na wazazi wenye uwezo mdogo kifedha wanawasiwasi na elimu wanayopata watoto wao.
Matokeo ya utafiti huu uliohusisha sampuli ya wazazi 250 kutoka wilaya tatu za mkoa wa Dar es Salaam unathibitisha ukweli ambao tunaujua kwa hisia zetu, kwa kusoma na kufuatilia vyombo vya habari, ukweli kwamba elimu yetu imeanza kujenga matabaka kati ya walio nacho na wasio nacho. Ifuatayo ni sentesi toka kwenye taarifa ya utafiti huo.
 Utafiti pia umeonyesha wazazi tajiri huridhishwa na shule wanazosoma watoto wao zaidi ya wazazi ambao si tajiri.Katika kipimo cha juu cha utajiri cha waliohojiwa,45.6% wana mtazamo chanya kuhusu elimu ya watoto wao, wakati 21.9% ya wazazi waliopo kwenye 20% ya kipimo cha chini cha utajiri waalitoa tathmini chanya juu ya shule wanazosoma watoto wao .Imeonyesha kwamba wazazi wenye uwezo wa kifedha kupeleka watoto wao shule binafsi pia wameridhishwa na kiwango cha elimu wanachopata watoto wao.
 Utafiti pia unaonyesha kuwa wazazi wanatambua na wanakubali kwa dhati mchango mkubwa wa walimu katika elimu ya watoto wao. Theluthi mbili (67.2%) wamediriki kusema kuwa badala ya kuboresha majengo ya shule na kuongeza idadi ya vitabu na madawati katika shule, ni bora zaidi serikali ilenge kuhakikisha walimu wanapata mafunzo mazuri na kupata motisha katika kufanya kazi yao. Matokeo haya yanatoa mtazamo kwamba wazazi wanajali sana kuhusu ubora wa elimu ya watoto wao.
Na:Mkama Mwijarubi

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.