MTANGAZAJI

WABUNGE WA CHADEMA WATOLEWA BUNGENI LEO

Naibu Spika Job Ndugai akiwaamuru wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu, Mchungaji Peter Msigwa na Godbless Lema kutoka ndani ya bunge leo mara baada ya wabunge hao kudaiwa kuvunja kanuni ya bunge ya kuongea bila ruhusa ya Naibu spika.

Askari polisi wa bunge wakiwasindikiza Tundu Lisu(Kulia)Mchungaji Peter Msigwa (Kushoto) na Godbless Lema (katikati) watoke nje ya viwanja vya bunge mara baada ya Naibu spika Job Ndugaikutoa amri hiyo wakati wa bunge asubuhi ya leo.Picha zote toka Manaseblog
Kwa mara ya nyingine wabunge wa CHADEMA wametolewa bungeni leo ambao ni Mhe. Godbless Lema, Mchungaji Peter Msigwa na Mhe Tundu Lissu. Wametolewa bungeni katika bunge linaloendelea, sababu za kuondolewa kwao ni kuwasha vipaza sauti bila ruhusa na aliyewatoa ni naibu spika Job Ndugai.

Hilo limetokea baada ya kuibuka mvutano baina ya Wabunge, kutokana na hotuba ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Mhe Lema iliyoelezea ukiukwaji wa haki za binadamu zinazofanywa na jeshi la Polisi  nchini kwa ajili ya kutii maagizo ya chama tawala, pamoja na matatizo mengine ya idara za Wizara ya mambo ya ndani.

Baada ya hotuba hiyo Mheshimiwa Lukuvi alikerwa na kuiombea muongozo ambao kwa kuwa ulikuwa na maelezo ulianza kukera Wabunge wa upinzani na moja kwa moja kuanza kuhoji kama Mhe. Lukuvi anatoa maelezo ya kuomba muongozo au anatoa hotuba, jambo lililoibua vurugu bungeni na mabishano ya wabunge wa upinzani na chama tawala.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.