MTANGAZAJI

TIBA YA BABU YAANZA KUONESHA "MADHARA"

Maggid Mjengwa
INAYODAIWA kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeanza kuonyesha madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu sasa ni mradi, na kwa kweli umeanza kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa.

Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi mabaya, na ni sugu. Ndio, miongoni mwetu kuna wenye kusumbuliwa na maradhi ya unafiki. Nitatoa mfano wa juzi tu; nilikaa na wasomi wawili, tena wana digrii zao. 

Tukazungumzia ya Babu wa Loliondo. Mimi na wasomi wale tulikuwa na misimamo ya kufanana, tulipinga upotoshaji unaoendelea katika jamii kuwa Babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapile , anatibu ukimwi, kansa, kisukari na mengineyo. Na kwa vile wote tumekwenda shule, hoja kuu ilikuwa hii; kuwa hadi sasa hakuna hata wagonjwa watatu wa ukimwi waliothibitishwa kitaalamu kuwa wamepona ukimwi kwa dawa ya Babu. Badala yake, kuna wengi wamekufa baada ya kuacha kutumia madawa waliyoelekezwa na madaktari watalaamu waliosomea tiba.
Kwa maelezo zaidi bofya hapa

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.