MTANDAO WA FACE WAONGOZA KUVUNJA NDOA
Kutokana na vishawishi vya kimapenzi kutokana na picha na meseji zinazoandikwa kwenye Facebook zimepelekea watu wengi wazisaliti ndoa zao na matokeo yake kumekuwepo na ongezeko kubwa la kuvunjika kwa ndoa chanzo kikubwa cha kikiwa ni Facebook. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni kuhusiana na matumizi ya mtandao wa Facebook umeonyesha kuwa ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na wanandoa kuingiwa na vishawishi na baadae kuzisaliti ndoa zao kwa kuanza mahusiano ya kimapenzi na watu wanaokutana nao kwenye mtandao huo mkubwa duniani. Utafiti uliofanywa nchini Uingereza umeonyesha kuongezeka kwa kasi ya kuvunjika kwa ndoa kutokana na watu kufumaniwa wakiwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa na watu wanaokutana nao kwenye Facebook. Mwanasheria mmoja wa masuala ya familia alidokeza kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, alizisimamia kesi 30 za kuvunjika kwa ndoa na kesi zote zilihusisha mtandao wa Facebook kama chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hizo. Mwanasheria mwengine alisema kuwa katika kila kesi tano walizozisimamia za madai ya talaka, kesi moja ilihusisha mtandao wa Facebook kama sababu kuu ya kuvunjika kwa ndoa. Emma Patel, mwanasheria wa kampuni ya Hart Scales & Hodges Solicitors, alisema kuwa tovuti ya Facebook imegeuka kuwa mtu wa kati wa kuzitenganisha ndoa za watu. “Facebook imekuwa ikilaumiwa kwa ongezeko la kuvunjika kwa ndoa na cha kustaajabisha katika kesi zote nilizozisimamia tangu mwezi mei mwaka jana zote zilihusisha tovuti ya Facebook kwa njia moja au nyingine”, alisema Emma. Miongoni mwa watu waliovunjwa mioyo yao kutokana na mtandao wa Facebook ni James Wrigley, 34 wa mjini London ambaye alisema: "Mpenzi wangu alinitosa baada ya kugundua kuwa nilikuwa nikiwatumia meseji kwenye Facebook wanawake niliokuwa nikifanya nao kazi”. “Alipata password yangu ya Facebook, alisoma meseji zangu zote na huo ndio ukawa mwisho wa uhusiano wetu wa miaka mine, sijahuzunika sana kwa sababu hatukuwa tumeoana”, aliongeza James. Mfano mwengine ni mama wa mtoto mmoja, Marianna Gini, 32, ambaye ndoa yake ya miaka sita ilivunjika baada ya kugundua kwa kupitia mtandao wa Facebook kuwa mumewe Robert, 34, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwengine nje ya ndoa. Mwanamke mwingine wa nchini humo aliamua kuvunja ndoa yake na mumewe baada ya kugundua mumewe alikuwa akimtumia ujumbe wa kimapenzi mwanamke mwingine ambaye hata hawakuwahi kukutana. Msemaji wa Facebook alipoulizwa kuhusiana na lawama wanazotupiwa Facebook za kuvunja ndoa za watu alijibu kwa kusema “Ni sawa na kuilamu simu yako ya mkononi au email yako”. “Kwani kuingia kwenye Facebook mtu hulazimishwa kufanywa kitu asichokipenda? , jibu lingekuwa ni Hapana.”, alimalizia kusema msemaji huyo wa facebook | |||||
Kutoka:www.nifahamishe.com |
Post a Comment