MTANGAZAJI

UJAMBAZI WA AJABU DAR ES SALAAM

Ndugu Watanzania kumezuka Ujambazi wa ajabu hapa Jijini Dsm.
Juzi tarehe 17//3/2010 Jirani yangu alikwenda Benki kuchukuapesa majira ya saa 10:00 jioni Mjini.Baada ya kuchukuwa pesa zake alielekea kituo cha Basi kusuburiBasi.

Akiwa kituoni hapo akashtukiwa mama mmoja anamfuata na kusemandiye huyu.Wakajitokeza na wanaume wengine wakamkamata yule mama akasemasogeza gari hapa, Huku akienddelea kumtukana mtuhumiwa.

Wakamwambia sisi ni polisi Vitambulisho hivi hapa.Akaingizwa kwenye gari ndogo inayosadikiwa kuwa ni ya majambazihayo.Haya twende POLISI KATI gari ikaelekea polisi cha ajabu palepolisi ilipitiliza akapelekwa hadi Tandika.

Kule walimnyang,anyapesa zote, Wakamwambia sasa tunakupeleka POLISI KATI, Tandikawalikaamuda mrefu.Mtuhumiwa akawaomba hao polisi Fake wamruhusu awapigie ndugu zake.Wakakubali akawapigia Ndugu zake kuwa amekamatwa kwa tuhuma yaujambazi na anapelekwa kituo cha polisi kati.

Ndugu zake walimfuatilia hadi Kituo cha polisi kati na hawakumkuta.Baadae kule Tandika Majambazi hayo yakamwambia Mtuhumiwa kuwaSasa tunakupeleka kituo cha polisi kati.Wakaondoka hadi maeneo ya Buguruni Mtuhumiwa akashangaawanaelekea Ubungo, Walipofika SUKITA majambazi hayoyakasimamisha gari na huku yakiwasiliana na mwenzae kuwa yule mtutumemkamata njoo tuelekee Kimara.

Muda huo walijisahau wakafungua Mlango wa gari wakawawanazungunza kwa nje kidogo.Jirani yangu huyo alichumpa kutoka ndani ya gari akatoka nje nakuanza kupigana na majambazi hayo.

Aliyashinda nguvu yakawasha gari na kukimbia, Hata hivyoalibaki na maumivu makali kwakuwa walimpiga na kitu kizitomgongoni.Gari moja ya Raia mwema ilipita na kumchukua hadi polisiBuguruni muda huo ikiwa ni saa 1:30 ujioni.

Polisi Buguruni walimwambia Jirani yangu kuwa una bahati Watuwatu tayari walishaokotwa wakiwa wamekufa huko Kimara.Na wewe ni mtu wa pili kunusurika, Pole sana.

Wananchi tujifunzeni mtu akituhumiwa kuwa ni Jambazi mbele yakemaana yake ni kukufunika wewe usijue wanatakakufanyanini?Kwa hali hiyo kuanzia sasa tuwe makini na kuwaeleza marafiki naJamaa.Ukisikia Mtu anasema huyu ni jambazi ujue anaibiwa na wakimwibiahuyo bado na wewe siku yako ya kuibiwa na huku watu wakidhani kweliwewe ni jambazi.Naomba hatua za makusudi zichukuliwe.

Jirani rangu huyo hado leo anaugulia maumivu makali sana.

Mdau Rashid Varisangas

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.