MTANGAZAJI

NENO KABLA YA IT & COMMUNICATION SUMMIT 2010

Wakati ambapo Watanzania wakijiandaa na Ufunguzi wa IT &Communication Summit , Nchini Kenya wiki hii Kumefunguliwa kituo chaTEKNOHAMA ambapo wadau mbalimbali wa Fani hiyo wanaweza kwenda kutumiavifaa vya vituo hivyo kwa ajili ya kazi zao mbalimbali haswa kwawanafunzi ambao wanahitaji kufunza zaidi na wale wanaopenda kujiajiriwenyewe mradi huu uko chini ya Ushahidi.com Hii ni hatua nzuri sanakwa Kenya na afrika mashariki kwa ujumla .Pia Kampuni kadhaa za mawasiliano ya mtandao yameahidi kusaidia katikakuhakikisha kituo hicho kinapata huduma ya mawasiliano bure kwa sikuzao zote za kazi .

Uganda napo serikali ya nchi hiyo itaanza kuwapa ardhi bure wadau waTEKNOHAMA lakini hii itafanyika kwa wale wenye miradi inayoeleweka yakibiashara ambayo inaweza kusaidia jamii za sehemu ambapo mdau husikayupo haswa vijijini na sehemu zingine ambapo teknologia hii iko nyumakidogo hii itakuwa changamoto sana kwa wadau mbalimbali wan chi hiyokuja na mawazo miradi na mambo mengine kwa faida ya jamii zao .

Mambo hayo yakiwa yanaendelea kwenye nchi za wenzetu tena jirani zetukuna mambo ambayo sisi kama watanzania yatupasa kujiuliza mipango yetuya TEKNOHAMA mpaka sasa hivi inaendeleaje je yale ambayoyalipendekezwa miaka 5 iliyopita yamefikia malengo au kutekelezwa hatakidogo tu tunaweza kuona nyota njema ikingaa mbele zetu ?

Kwa kuanzia tunaweza kuangalia upya kama TCRA Taasisi inayohusika namawasiliano nchini kwa ujumla kama imeweza kufikia malengo yakeiliyojiwekea na kama bado inafaida kwetu kama taifa au kuwe na taasisinyingine mama iliyohuru katika utendaji wake wa kazi mbalimbalizinazohusu mawasiliano , kwa kweli Hii Taasisi ni ya kuangalia kwamacho makali , lazima ifanyiwe mabadiliko ili iwe ya kisasa iwezekuendana na wakati wa sasa kwenye Sekta ya Mawasiliano Kuna hitajikaplatform Mpya ya kuendesha mfumo mzima wa mawasiliano Nchini

Imeonekana Umeme kuwa Tatizo sugu sana katika utendaji wa Masualamengi ya TEKNOHAMA , hapa ninapoandika hii barua fupi niko Katikati yaJiji zaidi ya Nusu ya Jiji lote la DSM halina umeme kwa masaa 4 sasana hali hii imekwepo toka mwaka jana hii ina maana shuguli nyingi zateknohama haziwezi kuendelea kama ilivyo labda kwa wale wenye uwezo wakuwa na vifaa vya kuzalishia umeme lakini hii inaweza pia ngumu kwawale wasiokuwa na uwezo .

Kitu cha mwisho ni kwa wadau mbalimbali kufikria sasa kuwa na Contentszinazohusu mambo yetu kwenye wavuti zao suala hili limeonekana kuwagumu kwa wengi wetu lakini naamini siku zijazo kunaweza kuwa namabadiliko makubwa tukiamua kuwa na contents zetu .

Na ushirikiano kati ya watu wa TEKNOHAMA Umekuwa hafifu sana wengihawaaminiani - Hili siwezi kuliongelea kwa mapana lakini nawaombawana TEKNOHAMA tuzidishe ushirikiano wa kazi za kila siku ili tusogezetaifa hili Mbele ,Lakini kutokuwepo Taasisi ya kutambua wataalamumbalimbali kwenye TEKNOHAMA imechangia sana suala hili .

FRED MARO

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.