MTANGAZAJI

UNAMLINDAJE MWANAO NA MTANDAO

Mwaka jana kwenye wiki ya TEKNOHAMA neno kuu lililotumika ni MKINGEMTOTO NA MITANDAO ,mambo mengi sana yalijadiliwa kwenye wiki hiyo yaTEKNOHAMA huu ni mwaka mpya sasa nimejaribu kuangalia kuona jinsiwazazi wanavyozingatia hili la kukinga watoto wao na mitandao .

Wengi ninaowaona kuongea nao au kujadiliana masuala mbalimbaliyanayohusiana na Mitandao wamewekeza sana katika vitu kama programu zakurekodi kila kitu ambacho motto wake anachofanya kwenye mtandao kwawakati Fulani yaani kuhifadhi taarifa zote .

Wengine ni kuweka muda maalumu wa kutumia kompyuta kuingilia kwenyemtandao huku yeye mzazi akiwa pembeni kuona mtoto wake anachofanya ilikujaribu kumfundisha haya na yale .

Kundi lingine ni lile linalokataza watoto wao kutumia kitu kinachoitwakompyuta kabisa majumbani mwao mpaka watoto wao wafikie umri Fulanilakini hawa watoto inawezekana wakatumia kompyuta hizo mashuleni mwaoau kwa rafiki zao au mitaani tu .

Na la mwisho ni hili ambalo limeamua kununua michezo ya kompyuta kwaajili ya watoto wao watumie muda mwingi katika kucheza michezo hiyokwenye kompyuta zao .

Kwenye makundi yote hayo pia inategemeana na hali ya kiuchumi ya mzazihusika sio hilo tu na hata watoto hao wako kwenye mazingira gani ilikuweza kupata nafasi ya kutumia vifaa hivyo au hata kuviona vikifanyakazi naamini wengi watakuwa ni wale wa maisha ya kati na juu .Juzi nilikutana tena na mmoja wa wazazi hawa yeye amempa mtoto wakewa miaka 16 kila kitu kuanzia kompyuta iliyounganishwa kwenye mtandaomuda wote simu na vifaa vingine kwa ajili ya matumizi yake .

Mzazi alianza kuona mtoto wake mambo yanabadilika kidogo akaamuakumwomba password yake ya anuani ya barua pepe ili aweze kuona kileanachoandikiana na wenzake ,mtoto kuona hivyo akawa anafuta kilaanaposoma .

Yule mzazi akaamua kuforwad barua pepe zote zinazoingia kwenye anuaniya mtoto wake kwenda kwenye anuani yake bila mtoto Yule kujua piakujiunganisha kwenye simu yake ya mkono ili aweze kusikilizamazungumzo pindi mtoto wake anapoongea kwenye simu .

Nilijaribu kuangalia kwa mfano watu alio nao kwenye mtandao wafacebook niligundua majina kama 3 hivi lakini moja ndio nilikuwanalijua ni la mtu wa miaka zaidi ya 45 aliyekuwa anajaribu kupatamawasiliano ya mtoto wa miaka 18 kwa kumbembeleza…..

Suala la kumkinga mwanao na matishio mbalimbali ya mtandao ni zaidi yakuhifadhi mazungumzo anayoyafanya kutumia kompyuta na vifaa vinginevya mawasiliano kama ukirekodi ya nyumbani anaweza kutumia yashulenikwao kwa raha zake kwa mfano au anaweza kwenda kwa jirani au anawezakwenda kwenye mgahawa wa mtando na kufanya shuguli zake .

Je wewe kama mzazi unafanya nini kumdhibiti mtoto wako na matumizi yakompyuta haswa anapotembelea mitandao mbalimbali duniani ? kamahatembelei akiwa nyumbani kwako anatembelea shuleni tu je unajua seraya TEKNOHAMA ya shule anayosoma mtoto wako umewahi kuisoma nakukubaliana na kitu kilichoandikwa humo .

Niliwahi kutembelea shule moja mjini arusha ( Arusha Modern ) Hiishule haina Sera ya TEKNOHAMA kwenye chumba chao cha kompyutawanafunzi wanaweza kufanya chochote wanachotaka kwenye kompyuta hizokuanzia kutembelea mitandao mbalimbali , kushusha vitu na kuwasilianana wenzao popote walipo huu ni mfano halisi wa mambo yanayoendeleanyuma ya pazia , kwahiyo kama mzazi ni muhimu kujua sera ya Teknohamaya shule anayosoma mtoto wako uchukuwe uisome na kuweka sahihikukubaliana na kile kilichomo ndani .

Kuhusu kutumia program za kuhifadhi kila anachofanya mtoto wako kwenyekompyuta na mitandao hii kwangu sioni kama ni njia bora unawezakumfanya mtoto wako awe muaga asiwe huru kufanya anachotaka yeye na ningumu sana kwa yeye kujifunza baadhi ya vitu kama akitambuaanafuatiliwa kuheshimu uhuru na masuala binafsi ya mtoto wako nimuhimu sana lakini pia angalia na umri wa mtoto wako kabla hujaamuakumhusisha sana na masuala au matumizi ya kompyuta .


Siku hizi kuna mitandao jamii kama facebook , tagged, hi5 na menginemingi tu kama umeweka programu za kuzima au kufunga mitandao michafumtoto wako asiangalie basi anaweza kuingia kwenye mitandao jamii kamafacebook na hi5 akakutana na wahalifu humo ndani wakawasiliana nakubadilishana habari zingine mwisho wa siku mtoto anaweza kuumizwa .

Ni muhimu sana kuangalia wale watu ambao mtoto wako anawasiliana naokwenye facebook na mitandao mengine ya jamii ambayo imezagaaduniani ,kujua wale anaowasiliana nao kwa njia ya barua pepe nawengine wengi na kama kuna chochote unapenda kumfundisha mtoto wako aukumkataza uanzie na hapo lakini angalia usiingilie uhuru wake wakuwasiliana wala kuvunja haki zake zingine .

Hili ni jukumu la Wazazi na walezi huko majumbani kwa kushirikiana nawalimu mashuleni ,wahudumu wa migahawa ya mtandao pamoja na wadauwengine kutengeneza njia mbalimbali zinazoweza kusaidia pandembalimbali kwenye suala hiliHaya ni mawazo yangu tu wewe kama mzazi na walimu mashuleni muna mengizaidi .

Yona F Maro

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.