MTANGAZAJI

MATAPELI WA INTERNET

Kuna email inatumwa ikiwa na subject ya "Yahoo Update" au "Gmail Update" au "Hotmail Update". Hii Email inauliza User Name, Password, Birth Date, na Country.

Tafadhali usijaze wala kuijibu email hiyo.

Ni watu wanaofanya biashara ya utapeli. Ukijibu email hiyo, hutaweza tena kufungua email account yako tena. Password yako itabadilishwa, na email account yako itapata mmiliki mpya ambaye ataanza kuifanyia biashara za kitapeli.

Rafiki zako watatumiwa email kwamba umekwama nchi fulani, na unahitaji msaada wa kifedha. Tafadhali kuwa makini sana .

TAHADHARI:
Pia usipende kujiregister katika mitandao usioelewa wanamadhumuni gani, especially wanaotoa offer za vitu au pesa, ni geresha tu na wanajua mwishowe wakikuomba password utatoa ile unayotumia katika mail address yako, msidanganyike!!

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.