MTANGAZAJI

SIJAONA TIMU YA KUTUTOA KIMASOMASO WAAFRIKA KWENYE WORLD CUP 2010

Ndugu zangu!
Mim ni mmoja kati ya wapenzi wa soka ambaye nilikuwa na matumain makubwa kuwa huu ni mwaka wa Afrika kufanya "wonders" kwenye fainali zitakazofanyika huko bondeni kwa Mzee Mandela.

Nilianza hata kujinyima angalau nikaangalie baadhi ya mech nikitumain walau timu mbili zitafika hatua ya nusu fainali!Lakin baada ya kushuhudia wawakilishi wanne kati ya watano ( mwakilishi wa 6 ambaye ni mwenyeji ameshindwa hata kuvuka kwenye hatua za awali baada ya kufungwa na Zambia tena nyumbani kwa kipigo cha aibu)

Nachelea kusema timu zetu za Afrika zitakazotuwakilisha hazitoi matumain yeyote hata ya kuvuka tu kwenye makundi magumu waliyopangwaWalianza Algeria kufungwa 3-0 na timu ambayo ni mara ya 2 tu kushirik kwenye michuano hiyo ya Malawi, ikaja timu ya 2 kwa Ubora Africa ya Ivory Coast ambayo hata Mheshimiwa Rais ametutaka kuwashangilia lakin tukashuhudia wakichemsha mbele ya Bukina Faso.

Tukashuhudia Nigeria nao wakipata kipigo cha aibu mbele ya Misr na kocha wao akifanya mabadiliko ya ajabu ya kumtoa Ob Mikel kumuingiza Kanu wakati mchezaji aliyewafungia mabao mawil jijin Nairobi na kuwawezesha kushirik kwenye World Cup Obafem Martin akiwa bench!!!!Na mda mfup uliopita twashuhudia.

Timu inayoongoza kwa ubora Africa kwa viwango vya FIFA, Cameroon wakigagaduliwa na Gabon!Kwa soka hili na kwa viwango hivi sioni namna tutakavyowazuia kina Lionel Mess wa Argentina, Luis Fabiano na Kaka wa Brazil, Ronaldo wa Ureno, vijana wenye vipaji Lukuki i.e Inesta, Xav Hinandez, Fabregas, Torres, wa Hispania, bila kuwasahau mabingwa watetez Italy, Germany na Uholanz wasichukue kombe na kulivusha bahari kwenda kwenye mabara yao!

Yuko wapi yule Drogba anayeongoza kwa ufungaji magoli kwenye Barclays Premeur League na ambaye akiumia pale Chelsea makocha huchanganyikiwa? Samuel Etoo niliyemuona leo si yule aliyemgeuza kama chapati Vidic( wapenz wa Man U naomba mnisamehe bure) na kuifungia Barca bao la kuongoza kwenye fainal ya UEFA Champions League

Nadhani wengine watadai kuwa timu zetu bado zina mda wa kujirekebisha, lakin tukumbuke kuwa baada ya michuano hii wachezaji hawa watarud kuzitumikia klabu zao na watakusanyika tena wik 2 au 3 kabla ya World Cup na mastaa weng wakichelewa ( au wengine wakigoma kabisa Kama walivyofanya Suley Muntar na Michael Essien kugoma kucheza mech ya kirafik na Angola ) kujiunga kwa visingizio mbalimbal wakat kwa wenzetu Ulaya kina David Bekham na Patrick Viera wakihaha kupata nafasi za kuziwakilisha timu zaoJe, tatizo ni wachezaji wa Africa kukosa Uzalendo au ....!!??
WWR
GM-gm26may@gmail.com

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.