MTANGAZAJI

MTANDAO WA MATAPELI NI WA MUDA MREFU

 Nimeguswa na hili na kwa sababu ni 'point of pain' naomba kuwashirikisha na mimi kidogo tu kuhusu utapeli na wizi wa kimtandao. Mimi vile vile nimeingizwa mjini kupitia utapeli wa madalali wa nyumba za kupanga.

Jamaa walifika nyumbani kwangu na kuacha barua kuhusu nia ya wataalamu wa JICA kutaka kupanga nyumba etc. Ndugu zangu wakadanganyika baada ya kuona mikataba ikiwa na nembo zinazovutia. Tukatakiwa kufanya marekebisho kulingana na mahitaji ya mpangaji, na hao madalali wakajifanya wanaweza kushighulikia marekebisho hayo haraka ili kukidhi mahitaji kabla ya deadline ya kuonyesha nyumba hiyo kwa mabosi.


Unaweza kutabiri yaliyofuata lakini tuliingizwa mkenge. Jamaa hawa wanatembelea Tanzania nzima. Na tukio hili lilitokea Singida mimi mwenyewe nikiwa Mwanza.



Nimeriport jambo hili Police na nimepelekwa katika kitengo cha cybercrime. Kufuatana na utafati unaondelea tumeweza kuwatambua wahusika. Kwa vile wanatumia simu si vigumu kuwapata hata kama wakibadilisha line.



Kilichonistua ni kwamba jamaa wa mtandao huu wameanza shughuli hizi tokea 2003. Modus Operandi ni ile ile na wanatumia majina yale yale. Kufuatana na utafiti tuliofanya wamewahi kuwaibia watu wa aina zote - makasisi, watawa viongozi, wastaafu, wafanya kazi, wafanya biashara, wanawake kwa wanaume.

 

Majina yanayojitokeza katika mtandao ulioniathiri mimi ni:

1. Mr. D.A. Odhiambo
2. Mr. George Kachingwe
3. Mr. S.H. ole Sabai
4.Mr. Waltra Harbra
Wengine ni

1. Mr. Mzee Abdala (anajifanya ni Askari wa kitengo cha ukachero Makao Makuu Polisi DSM)- aka James Shebashi



2. Mr. Ephrahim Kajala (aajifanya ni askari upelelezi msaidizi wa 'Mzee Abdala') aka Kalonga Kalonga



3. Mr. Selemani Juma Kaboko - mwenye account NBC na anatumiwa na kundi hili kama mfereji wa kupishia fedha.

Jamaa hawa wanatumia majina ya watu na wanafanya utafiti wa kutosha kama kawaida ya matapeli wa kwenye mitandao. Kwa ujumla wao wanatumia jina la Japan- Tanzania Orphan Project wakipose kuwa inafadhiliwa na JICA. Katika makabrasha niliyoyaona jina hili hili la kampuni feki limetumika kwa zaidi ya miaka mitatu.



Jamani tuwe macho sana na atakayepata habari hii na amtaarifu ndugu jamaa rafiki na mwingine yeyote mwenye mapenzi mema. Kwa upande wangu kikubwa ni kujaribu kuvunja huu mtandao na nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu. Labda ni ndoto lakini nadhani nataka kufanya hivyo nione nitafikia wapi.

Wasaalam

JOSEPHINE LEMOYAN

16 comments

Anonymous said...

Your blog keeps getting better and better! Your older articles are not as good as newer ones you have a lot more creativity and originality now keep it up!

Anonymous said...

Nashukuru sana kwa taarifa, yaani hapa nilipo nini barua na hao matapeli, walitaka kuniingizza mkenge.

Anonymous said...

Dada Josephine nakushukuru sana kwa kutoa taarifa hiyo, sababu hao jamaa ni matapeli, na nashindwa kuelewa vyombo vya usalama vinashindwaje kuwakamata sababu wanatumia benki na mawasiliano mengine kama simu n.k.

Dada yangu keep it up, tunahitaji watu kama nyie katika jamii.

Ni mimi Davis.

Anonymous said...

Dada Josephine ningepata namba yako ningekutafuta maana mimi wameniletea barua na wewe ndio umeniokoa. Ninatamani mno wakamatwe maana hadi sasa wanaamini wamenipata.

Anonymous said...

Duh, mimi nimeombwa hela na hawa jamaa wakijidai wanaleta hao wajapani. Nilipowaambia kuwa kuna mtu atawaletea hela wakagoma kadai nisuri tu siku hizo 45.

Anonymous said...

Duh, mimi nimepokea barua ya hao matapeli tena nilikuwa nimeanza mawasiliano nao. Ilifika wakati wa kulipa ndo wakaniomba laki 3 ili wahonge TRA kibali cha kusamehewa kodi kitoke mapema. Kilichofanya nistuke ni baada ya kuletewa jina la mtu mwingine na AC ya Bank.Eti ni secretary wao. Ukiwauliza officsi yao iko wapi umpelekee akakata simu.

Anonymous said...

Hawa jamaa bado wapo jamani. Na sasa wameongeza kasi sana Dar es salaam. Wanadanganya wamepat project mpya Madale, ndio wanatafta nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wao watakaokuja mwezi wa kwanza. Wenye nyumba kuweni makini sana! Mimi wameleta barua wiki iliyopita

Anonymous said...

He He He!!!!! My Godness! ni kweli kabisa dada Josephine. Nami yamenikuta! ni kweli kweli tupu. na simu nimewapigia!!! na sasa cha kushangaza e mail adress yao haifanyi kazi ambayo ni jataoro@yahoo.com.
Eti wanajidai wako Mwanza plot No. 555 Nyegezi.
Ahsante sana dada, mungu akubariki sana kwa kuniokoa nilitaka kuuvaa mkenge live!
Nami niliikuta tu barua ikiwa imetupwa ndani wakati kuna servant kota. Makubwa haya. Iko siku wataangazwa.
sasa wapo eneo la Salasala kilimahewa.

ni mimi Mr. H.Mmbaga.

Anonymous said...

Mmh ndugu zangu ni kwel hawa matapeli mimi mwenzenu nimeuvaa mkenge Morogoro na niliona ni wahitaji wa nyumba kweli na modus operandi waliyoitumia ni hiyo ya kuhonga TRA ILI MALIPO YAWAHI Wanatumia namba 0758409096 na 0682768889 Ole Sabai ni vyema watu wa usalama waingilie kati asante kwa kunifumbua macho na masikio kwani nilikuwa naendelea kufanya nao mawasiliano
Charles Dar

Anonymous said...

Hi dears
Mie pia nimekuta kibarua kama hicho wamepitisha kwenye pagale langu hapa moro, Wakionyesha mkataba ambao tayari uko approved kwa nyumba yangu. Mjini shule nikasema niangalie kama ni project kubwa ya JP itakuwa na website na hiki ndicho nilichoona. Majina ni ollesabai. Mkataba wa unono, usd 800, 600 na 400pm kulingana na class ya nyumba. Mambo hayo, Jamani mjini shule watu washauliwe kusoma sana na kutafuta ukweli kabla ya kuingia kichwa kichwa, Wasalaam

Anonymous said...

Teh teh teheeeee!!!!Jamani kweli mjini shule mimi yamenikuta nimekuta barua ndani ya nyumba na nimewasiliana nao ikafikia hatua ya kuwatumia hela sh laki 3 kwa ajili ya kuhonga TRA.ila baada ya kuona hivi nikasema hebu niingie kwenye website kuona kama kweli hii project ina exist...loooh ndo nikawakuta waungwana wenzangu.nachowaomba tuwe waangalifu sana kwani hawa watu ni wajanja sana.

Anonymous said...

jamani yamenikuta ni juzi walikuja kwenye eneo langu chanika ila sikufikia hatua ya kutoa hela walikuwa bado wapo kwenye mawasiliano na wakaniambia niende posta wamenitumia mkataba wa vitu wanayohitaji jamni tuweni mamcho mimi nashangaa kwa nini simu zimeshasajiliwa na hawakamatwi?nadhani kuna siri kubwa nadni ya mtandao huu..lakini siku moja watakamatwa tu.
Yaani ni jana tu ndio nimecheck mtandao nione ahiyo project ndio nakutana na watu wametoa comments zao kuwa wameshatapeliwa. Tuwemakini kwa kweli.

maisha dunia ngumu said...

mimi niko amerika, najenga nyumba yangu hapo dar, fundi anayejenga nyumba amenipigia simu kuwa watu hao wa TANZANIA ORPHARA PROJECT WA SIMU NUMBER 0783-927-196 MR SABAI wana hitaji nyumba ya kupanga kwa miaka 2 kwa dola 800 jumla watatoa dola 19,200.00 kwa ajili wafanyakazi wao, wakasema watajenga fence ya umeme kuzunguka nyumba, kuchimba kisima cha maji, watamalizia kuweka umeme kama offer . Lakini baada ya kupata habari hiyo nikapiga simu kwenye ubalozi wa japan hapa USA wakasema hakuna shirika la namna hiyo na wakanitajia majina kama hayo uliyoolezesha kuwa ndiyo wamiliki wa shirika hilo haramu.OK WANAIBAJE? watakupeleka kwa wakili wao ambaye pia ni taperi mwenzao, unasaini mikataba mingi usiyoilewa na kwa vile mawazo yako yote yako kwenye lundo la pesa ya miaka miwili unasaini tu, lakini akili yao ni kukusainisha mkataba kwamba unawauzia nyumba kwao kwa bei hiyo ya kupanga kwa miaka miwili, sasa kwa vile wewe hujui baada ya miaka miwili ya mkataba wa kupanga kuisha ukiwambia ku-renewal mkataba watakucheka kwamba wewe uliwauzia nyumba, na ni kweli umesaini tena kwa wakali!!! kuweni macho sana-maishaduniangumu@gmail.com

Anonymous said...

kwa sasa hawa jamaa wapo pia maeneo ya chanika, buyuni, mbande na mvuti. wanadai eti wanataka kujenga orphanage centre maeneo ya mvuti kwa hio wanatafuta nyumba za kukaa wafanyakazi wao. wakaazi wa viwanja vya mradi buyuni kuweni makini maana wamemwaga mibarua yao kibao maeneo hayo

Salum said...

MMh hii kali,maana hata nimeletewa hiyo barua ya hawa wazushi,nikaiangalia nikaanza sema na moyo wangu,hapana deal ya milioni 30 kirahisi hivi,mmh hapana,jamaa hawa ni hatari sana,maana kusema kweli sijui ni wangapi wameshaumizwa na wangapi watafuata lakini nashukuru sana kwa habari hii,nami nitavoluteer kufikisha ujumbe kwa wote.

Anonymous said...

poleni, mi nilikuwa napita tu lakini nimepata darasa. kweli mtandao unasaidia. Haki ya mtu haiendi bure, Mungu atawalipa.

Mtazamo News . Powered by Blogger.