MTANGAZAJI

MATUTA BARABARANI NI SULUHISHO LA AJALI TANZANIA??

Ndugu zangu wapenda maendeleo na mazingira mazuri. Hivi karibuni katika Nchi yetu ya Tanzania kuna ajali nyingi ´sana za barabarani. Hii kweli ni kero kwa Taifa na hasa wale wananchi walioko eneo husika la ajali. Bila kusahau si miaka mingi imepita tangu barabara nyingi na nzuri zijengwe katika Taifa letu. Miaka kama 20 iliyopita zilikuwa mbaya hazipitiki wakati wa mvua na ilikuwa ni kero kweli kweli. Ninatokéa kusini Mtwara, wanaojua wanaweza pata picha halisi.

Tumshukuru Mungu walao barabara nyingi kuu zimejengwa kwa kiwango cha lami na kupitika muda wote. Sasa tatizo linakuja tena. Madereva nao wanakuwa vichaa. Wanaendesha kwa kasi hata magari mabovu kwa sababu tu ya uzuri wa Barabara. Matokeo yake ni ajali za kila siku.

Wananchi nao wanakuja juu. Wanaona njia ya kunusuru maisha yao ni kujenga matuta katika barabara hizi. Waamechukua hatua hata kufunga barabara na kulazimisha serekali kujenga matuta hayo. Mfano´ni majuzi wananchi wa Mkuranga wameamua kufanya hivyo.

Mkuu wa Wilaya akaahidi pale pale kujenga matuta. Wanafunzi wa Chuo kikuu nao walifanya hivyo. Swali langu ni JE KUJENGA MATUTA BARABARA NI SULUHISHO?-

Kujenga matuta barabarani ni kuharibu manthari ya barabara- Kujenga matuta ni kuharibu magari- kujenga matuta ni kuongeza gharama zisizokuwa za lazima katika Taifa letu. Kaangalie matumizi ya Wilaya. Usishangae kuona Sh. Bil. 1 au zaidi zimetumika kujenga matuta barabarani. Kwa nini wasingetumia fedha hizo kununua madawati?-

Kujenga matuta ni kutotumia akili kukabili tatizo. Dereva hana akili mpaka awekewe matuta ili apunguze mwendo!Pendekezo langu.

Ni kufundisha madereva kutumia na kuheshimu ALAMA za barabarani. Kama mahali pameandikwa Km 80, 50, 30 kwa saa wafuate sheria hiyo.

Kama ni pa kusimama wasimame. Mbona kwa wenzetu wanaweza? Wanaweza kwa sababu wanafuata utaratibu na kufuata sheria za Barabarani. Je sisi Watanzania ni wagumu kiasi hicho au hatuna akili mpaka tuwekewe magogo barabarani ndipo tusimamame au tupunguze mwendo?

Katika nchi ya Ujerumani, alama za barabarani, namna ya kutupa takataka katika mapipa ya taka mijini ni somo linalofundishwa darasani. Na wanafunzi wanafanya zoezi hilo kwa vitendo. Hivi wanakua katika hali ya kujua alama hizo na kuziheshimu.

Ujerumani kama alama si ya kijani. Hata kama hakuna gari au mtu, mtu au gari havuki barabara. Anafuata sheria ya Alama. Na iwapo utavunja sheria hiyo hakika adhabu yake ni kali sana. Je serikali yetu imeshindwa kuweka sheria kali na kuzifuata hadi kufikia hali ya kuharibu barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa kwa kuweka matuta?

Jamani KUWEKA MATUTA BARABARANI NI KUHARIBU MAZINGIRA.
Mnasemaje?

Slyvanus Kessy

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.