KANISA LA WASABATO LATOA MATIBABU BURE ZANZIBAR
Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakisubiri kupata matibabu hayo
Kanisa la Waadventista Wasabato nchini Tanzania limetoa matibabu bure kwa wananchi wa Zanzibar kupita kituo chache cha afya kilichopo Meya,Zanzibar.
Akizungumza na blog hii Mkurugenzi wa idara ya Afya katika kanisa hilo kanda ya mashariki mwa Tanzania Dr Livingstone Kingu amesema zaidi ya shilingi milioni 4 za kitanzania zilitumika kununulia madawa kwa ajili ya matibabu hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku 3
Matibabu hayo yaliwahusisha wananchi wapatao 2700 kati yao watu 500 walipatiwa miwani baada ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya macho
Post a Comment