MTANGAZAJI

JIHADHARI NA UTAPELI HUU

Imemtokea mwenzetu

Ndugu wapendwa,
Story ifuatayo ni ya kweli maana imenitokea mimi binafsi jana tarehe11/11/2009. Najua kwa kiasi fulani itakuwa inaninizalilisha kwakutokuwa makini lakini naona ni vyema niwashirikishe rafiki zangu ilimsije mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa kama vilendugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza kutuelezea yaliyomsibu nduguyake labda na mimi ningeweza kuepuka utapeli huu.


Kinchosikitishamatapeli wenyewe ni watu wanaotufahamu vizuri.
Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo likizo) nikapokeasimu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye alijitambulisha ananifahamu,na kwa jinsi alivyonitaja kwa jina na career background details zangusikuwa na shaka kwamba hanifahamu.


Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.

Mimi: Nzuri

Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?

Mimi: Hapana, nani mwenzangu?

Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na uliwahikunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World food programme,Kigoma kama Chief supplies officer.

Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba sikumkumbuka ilakwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali, sikujiuliza sana, after all alikuwa hajasema anachotaka)

Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kamaunavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna maghala makubwaya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha vyakula haviharibiki huwatuna weka presavative inayoitwa Damoline Liquid solution made inSweeden, hii inapatikana MSD na kwa licensed dealers kama MohamediEnterprises. Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplieraliyeshinda tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayomadawa akanidhulumu na kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10%angeniripoti kwa mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya balikusubiri contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasandio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii kazi utawezakuifanya ukizingatia unalipwa cash on delivery!


NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi hivyo sikuwa nadoubt yeyote, bali nikaona hii is just another deal kama ambazonimeshawahi kufanya successfully.

Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?

Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr. Shija, huyundiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier wetu wa zamani aliye nidhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa kazi tena, wewe uende ujifanyeunaulizia hiyo liquid solution, na u negotiate ujue atakuuziashillingi ngapi. Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupequotation, alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya.

Basi wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitatekuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na strangers naakataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa kuwa siwezi kumwambiaukweli kuhusu aliyenipa namba yake, ikabidi na mimi niwe muongo kwamuda, nika pretend kuwa mimi ni mkulima na nahitaji hiyo presavativekwa ajili ya maghala yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani nakukiri kuwa anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair yachupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa angalianilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni kaomba punguzo naakasema atauza kwa 1million.

Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya kupata beinimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata ni kuwa mimi nitauzakwa USD. 1700, na tofauti kwa maana ya faida tutagawana, hivyonisubiri aniunganishe kwa bosi wake for further final details.

Basi wandugu kama mnavyonijua katika issue za fwedha, nikachukuacalculator ya simu ili nijue deal ina shillingi ngapi, helazilivyokuwa nyingi hata calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50pairs @ usd 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kamausd 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFUtunagawana pasu pasu.

Guys you can imagine what was going on in myhead!

Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake ambaye nimzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo:

MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new supplier?

MIMI: YES

MZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid solution, we arelooking for 50 pairs?MIMI: Yes I have sufficeint stock

Mzungu: what is your price per pair?

Mimi:$1700

Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to be paid indollars or TZS

MIMI: Dollar of course, you how how unstable the local currency is (Hapo tena na mimi nataka kuonyesha kuwa ni International businessman)

Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be paid cashor by cheque?

Mimi:Cash

Mzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new supplier weneed this liquid urgently possibly today, and since you have said youhave enoughstock we are taking off this morning from Kigoma coming to Dar, pleasearrange for the transport to take us to Movenpick, we will pay usd.200 for your fuel, but most importantly make sure you bring one pairof the sample with you.

Mimi: No problem at all I have been in this business for quitesometime now you can be sure everthing will be fine.

Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque book,nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample yakwendakuwaonyesha wateja wangu.

Baada ya kutoka bank nikampigia dr. shijaili aniuzie hiyo sample, akasema kwa sasa ametoka ofisini ila sampleanazo katika gari na alikuwa anaelekea Mwananyamala hosp, thenMagomeni alafu Muhimbili, hivyo tukutane Magomeni hosp.

Yaani jinsinilivykuwa naendesha gari basi hata kama ni mashindano ningewezakushinda, basi mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija.

Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi wakeasingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo fedha na yeyeanipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana akaja akaingia kwenye garinikamwambie anipe hizo sample kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFPwanavyotaka! NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION.

Bila hata aibu yule kijanaakaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa itakamilishwasaa nane.

Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri, nikampigiadreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza bei kutoka airportmpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000 nikamwambia usijali ntakupa50,000/=!!!!!!!!!!!!! (kumbuka mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri).

Basi mimi mbio nikaenda airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ilitumalize biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakunakitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi tenanikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride nikamsimulia jamaammoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza akasema hata ndugu yakeametapeliwa wiki iliyopita, nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yakealipigwa 3.5m last week.


Edwin

4 comments

Anonymous said...

mama weeeeeeeeeeee hii nayo kali!

MULHAT DORIA said...

mnhhh hiyo more fire,wadau tuwe makini jamani

MULHAT DORIA said...

jamani tujihadhari

Anonymous said...

Pole sana jamaa, ila ni vizuri sana habari kama hizi kuziweka hadharani, maana mjini hapa mambo ni mengi mno na matapeli ni wengi mno. Saa wamehamia kwnye kupangisha nyumba, wanajifanya Japan Tanzania Orphan Project, ni matapeli watuputu

Mtazamo News . Powered by Blogger.