MAMA SALMA KIKWETE "FIRST LADY" AENDESHA HARAMBEE YA KUCHANGIA SHULE YA WASABATO
Njozi za ujenzi wa shule ya Agape zilianza rasmi mwaka 2000 kwa andiko la mradi na hatimaye mwaka 2001 ujenzi ukaanza katika eneo kule liliko Kanisa. Mwaka uliofuata yaani 2002 shule ikaanza kwa kusajili watoto kwa ajili ya kuanzisha darasa la kwanza. Katika eneo hilo Kanisa lilijenga vyumba vine (4) vya madarasa, vyoo matundu 7 na ofisi moja ya walimu.
Agosti 29,2003 Mkaguzi Mkuu wa Elimu Manispaa ya Morogoro alipotembelea shule hii alishauri Kanisa liihamishe kutoka eneo hilo kwenda mahali pengine kwa kuwa eneo hilo ni dogo.
Hatua hii ilirudisha nyuma juhudi za Kanisa. Hata hivyo kwa kuwa lengo la kuwa na shule liliendelea kuwepo, Kanisa lilifanya jitihada ya kupata kiwanja kingine kipana chenye uwezo wa kutosheleza ujenzi wa shule. Kiwanja hicho kilipatikana katika eneo la Kitungwa.
Ujenzi mpya ulianza mwaka 2003 katika eneo hilo jipya. Ujenzi huo bado unaendelea hadi sasa. Shule ilipohamia eneo jipya tayari kulikuwa na wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili ambao walihamia kutoka eneo la awali.
Miongoni mwa wanafunzi hao walifanya mtihani wao wa darasa la saba mwaka jana, 2008.ambapo wanafunzi wapatao 10 waliomaliza darasa la saba wote walihaguliwa kujiunga na skondari,Mwaka huu 2009 wanafunzi wengine wamefanya mtihani, wanasubiri matokeo yao. Shule hiyo inahitaji kiasi cha shilingi milioni 100 ili kukamilisha ujenzi wa madarasa
Post a Comment