MTANGAZAJI

DR MBAKI ATUNUKIWA TUZO MAREKANI

Dk. Mbakisya Alinanine Onyango.

Leo nimevutiwa na kufurahishwa na habari hii iliyochapishwa kwenye gazeti la Nipashe la leo hapa nchini.Kutokana na ukweli kwamba Mbakisya(pichani) kama anavyojulikana na wengi kwa jina la Mbaki,mama huyu namfahamu kutokana na kuwa miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za injili hapa Tanzania na nakumbuka nilikutana na mama huyu nchini Uingereza akiwa safarini kuelekea Marekani kwa masomo mwaka 2004

Nipashe limeendika:

Mwanamke Mtanzania, Dk. Mbakisya Alinanine Onyango, ametunukiwa tuzo ya udaktari wa falsafa wa uhandisi wa ujenzi, iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Kansas State nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka nchini humo, Dk. Mbakisya, anakuwa Mtanzania wa kwanza mwanamke kupata tuzo hiyo.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa, Dk. Mbakisya, alitunukiwa tuzo hiyo Mei 15, mwaka huu katika fani hiyo ambapo msisitizo wake upo kwenye ujenzi wa barabara kuu.


Wasifu wa Dk. Mbakisya ulisomwa na Mkuu wa Idara ya Uzamivu wa Chuo hicho, Carol Shanklin.

Dk. Mbakisya, kabla ya kwenda Marekani kwa masomo, kama miaka minne iliyopita, alifanya kazi sehemu mbalimbali hapa nchini.

Baadhi ya nafasi alizoshika ni Msajili na Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha, Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) na mshauri wa muda katika kampuni ya COWI yenye makao makuu yake nchini Danish.

Kampuni hiyo ilishiriki ujenzi wa barabara ya kutoka Chalinze hadi Merera, ambapo jukumu lilikuwa kuongoza uchunguzi wa uwezekano wa kutumia udongo wa Polana kwa ujenzi wa barabara.


Dk. Mbakisya aliwahi kusoma Shule ya Sekondari Jangwani, alipata shahada ya kwanza ya uhandisi wa barabara kuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1992.

Pia alipata shahada ya uzamili katika fani hiyo kwenye Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza mwaka 1995. Chuo Kikuu cha Kansas City kimempatia Dk. Mbakisya nafasi ya kufundisha chuoni hapo ambapo anatarajia kufanya kazi hiyo kwa muhula mmoja tu, kisha atarejea nyumbani.

Wakati huohuo, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Ombeni Sefue, ametuma salaam za pongezi kwa Dk. Mbakisya, kufuatia kutunukiwa tuzo hizo. Miongoni mwa wageni waliohudhuria sherehe hiyo ni wazazi wa Dk. Mbakisya, Mwalimu Alinanine Mwambogela na Mwalimu Onika Mwambogela.

CHANZO: NIPASHE


BLOG HII INATOA HONGERA KWA DR. MBAKISYA

4 comments

Anonymous said...

Hongera zake dada yangu huyu. Katika wanawake mashujaa na wapiganaji I can say she's one of them. She deserves this. Hongera sana dada Mbaki.

Anonymous said...

Dada mbaki ameonyesha changamoto kubwa sana ya elimu kwa wanawake hivyo wanawake hawatakiwi kubweteka kwani mafanikio hayaji bure bila ya kugangamala.

emantu said...

Natoa shukrani zangu za dhati kwa Dr Mbaki. kwani namfahamu vyema tangia akiwa katika chuo cha Ufundi Arusha, nikama tulikuwa majirani, Temekuwa tukisali kanisa moja, Burka Sda Church.

kweli ni mwimbaji mzuri nami niliwahi mpigia kinanda wakati fulani kanisani. Dr Mbaki ameleta changamoto kubwa kwa wanawake... Wanawake wajue wanaweza kila kitu. Nimefurahishwa sana sana na ushindi wake huu mkubwa kwa taifa letu la Tanzani. Taifa changa.

Mimi,

Emmanuel M. Kiondo
kiondo@in.com

emantu said...

Natoa shukrani zangu za dhati kwa Dr Mbaki. kwani namfahamu vyema tangia akiwa katika chuo cha Ufundi Arusha, nikama tulikuwa majirani, Temekuwa tukisali kanisa moja, Burka Sda Church.

kweli ni mwimbaji mzuri nami niliwahi mpigia kinanda wakati fulani kanisani. Dr Mbaki ameleta changamoto kubwa kwa wanawake... Wanawake wajue wanaweza kila kitu. Nimefurahishwa sana sana na ushindi wake huu mkubwa kwa taifa letu la Tanzani. Taifa changa.

Mimi,

Emmanuel M. Kiondo
kiondo@in.com

Mtazamo News . Powered by Blogger.