MTANGAZAJI

WICHITA NDANI YA MOROGORO

Mara nyingi huwa najiuliza kwamba utakuta sehemu nyingi huku Afrika zimepewa majina ya nchi za nje,Je huko ughaibuni niambieni kuna sehemu nyingi zilizopewa majina ya kutoka bongo?hili ni duka pekee la kubadilishia fedha lilipo katika jengo la Posta Mkoa wa Morogoro

2 comments

Mbele said...

Ni suali zuri hilo. Ila jibu lake si rahisi. Ukifanya uchambuzi kutumia nadharia kama za akina Frantz Fanon, utaona kuwa sisi watu tuliowahi kutawaliwa na wakoloni bado tuna tatizo la kasumba, ambayo ni sehemu ya ukoloni mambo leo. Ndio maana tunashabikia vitu vya ughaibuni.

Lakini, suala haliishi hapo tu. Kuna vipengele vingine. Kwa mfano, hapa Marekani, Waafrika sehemu mbali mbali wanatumia majina ya kutoka Afrika kwenye biashara zao. Usishangae ukikuta maduka au migahawa yenye majina kama Kilimanjaro, Blue Nile, Addis, Benaadir, na Red Sea.

Wamarekani Weusi wengi wanafanya hivyo pia. Utakuta wana maduka, migawaha, au biashara zingine zenye majina kama Nubian, Timbuktu, na kadhalika.

Unknown said...

Ni kawaida tu hiyo coz wenze2 walisha2tangulia na wali2tawala so cc 2nawaiga.Sasa Sekulu cc ana2jua nani huko?

Mtazamo News . Powered by Blogger.