MTANGAZAJI

KIONGOZI WA WAADVENTISTA ULIMWENGUNI ATOA WITO KUOMBEA TANZANIA


 

 
 Kiongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji  Erton Köhler, Agosti 24, mwaka huu ametoa wito duniani wa kuomba kwa ajili ya Tanzania ambayo ni sehemu ya Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati, mojawapo ya maeneo makubwa zaidi ya Kanisa la Waadventista duniani.
 
 Köhler, raia kutoka Brazil, alichaguliwa kuongoza Kanisa la Waadventista wa Sabato duniani lenye makao yake makuu Silver Spring, Maryland, Marekani  Julai 2025, wakati wa Mkutano Mkuu wa 62 wa Kanisa hilo  uliofanyika St. Louis, Missouri ametoa wito huo kupitia mitandao yake ya kijamii ya Instagram na Facebook ambapo aliandika ujumbe huo akieleza kuwa Mungu na aitie nguvu kanisa lake linapobeba injili ya milele kwa wale ambao bado wanahitaji kuisikia.

"Takribani watu milioni 70 wanaishi Tanzania. Miongoni mwao, kuna takriban Waadventista Wasabato milioni 1.20 wanaoabudu katika zaidi ya makanisa 5,000 nchini kote. Tanzania ni sehemu ya Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati, mojawapo ya maeneo makubwa zaidi ya Kanisa la Waadventista duniani. Uwepo huu mkubwa ni sababu ya kushukuru, na pia ni mwito wa kuendelea kusonga mbele katika utume.
 
Leo, tuombe kwa ajili ya Tanzania. Mungu na aitie nguvu kanisa Lake linapobeba injili ya milele kwa wale ambao bado wanahitaji kuisikia. “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa tukimwomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.” 
1 Yohana 5:14 (NKJV). Kila kanisa na libaki kuwa kituo hai cha tumaini, likiwaongoza watu wengi zaidi kwa Yesu" 
 
  Köhler anawafuasi wanaomfuatilia kwenye Facebook wapatao 47,000 na Instagram 127,000,  akiongoza Kanisa la Waadventista wa Sabato lenye waumini  24,372,139.  kwa mujibu wa takwimu za Disemba 31,2025 zilizotolewa na ofisi ya Kumbukumbu, Takwimu na Utafiti ya Kanisa hilo (ASTR).

 

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.