COLOMBIA YATIKISHWA : WAADVENTIST WATHIBITISHA USALAMA WA WAUMINI.
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa Richter 7.4 liligonga eneo la magharibi mwa Colombia mnamo saa 1:34 asubuhi kwa saa za huko, Jumatatu, Agosti 10, na kusababisha vifo vya watu wapatao 111 na kuwajeruhi wengine kadhaa, kwa mujibu wa Reuters.
Tetemeko hilo lilikuwa karibu na San José del Palmar, Chocó, na lilisikika katika maeneo mengi ya Colombia pamoja na sehemu za Ecuador na Panama. Majengo yaliharibika au kuporomoka katika jamii kadhaa huku vikosi vya uokoaji vikiendelea kuwatafuta manusura.
Katika taarifa ya awali iliyotolewa saa 5:00 asubuhi Jumatatu, Henry Beltrán, Mwenyekiti wa Unioni ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Kusini mwa Colombia, alisema hakukuwa na taarifa za vifo au majeraha makubwa miongoni mwa waumini wa Kanisa la Waadventista. Viongozi wa kanisa walikuwa wakiwasiliana na viongozi wa Konferensi wa maeneo mbalimbali ili kupata taarifa kuhusu waumini, wachungaji, wafanyakazi, makanisa na taasisi.
Unioni hiyo iliripoti uharibifu wa miundombinu katika Shule ya Waadventista ya Cali, lakini wanafunzi walikuwa salama, wakiwa na familia zao. Unioni ya Kusini mwa Colombia inasimamia zaidi ya makanisa 800 yenye takribani waumini 110,000 katika eneo kubwa la kusini na katikati mwa Colombia.
Shirika la Misaada wakati wa majanga la Waadventista Duniani (ADRA) nchini Colombia pia limeanzisha utaratibu wake wa dharura lilieleza kuwa linafanya kazi na serikali, mashirika ya usimamizi wa majanga, na washirika kutathmini mahitaji ya kibinadamu.
Viongozi wengine wa Waadventista nchini Colombia na nje ya nchi pia walitoa taarifa na wito wa maombi. John Bradshaw, rais wa kituo cha Televisheni cha It Is Written cha nchini Marekani, ambaye kwa sasa yuko Colombia, alichapisha video inayoonyesha uharibifu wa tetemeko kwenye hoteli alikofikia, ikiwemo vipande vya dari na vifaa vya ndani vilivyoanguka wakati wa tetemeko.
Konferensi ya Pasifiki ya Colombia (Asopacífico) pia ilieleza kuwa inawasiliana na wachungaji na makanisa mahalia, huku Konferensi ya Texas ya Waadventista wa Sabato ikiwa miongoni mwa taasisi za kanisa nje ya Colombia zilizotoa wito kwa waumini kuombea kwa ajili ya waliopoteza wapendwa wao, waliojeruhiwa au kuhamishwa, pamoja na wahudumu wa dharura wanaohudumia wakati huu.
Idadi ya vifo bado ni ya awali na inaweza kubadilika kadri shughuli za uokoaji zinavyoendelea.

.png)
Post a Comment