MTANGAZAJI

MAMA ALIA NA SHIDA YA AKILI YA MWANAE ALIYEFANYA MAUAJI

 


Mama wa Mwanamume mwenye umri wa miaka 40 ambaye aliwapiga risasi watu wanne katika mauaji ya halaiki ya 31 kwa mwaka huu anasema mwanae alihitaji msaada wa kiakili kwa takriban muongo mmoja lakini familia yake na maafisa hawakuweza kumlazimisha kupata matibabu.
Andre Longmore alipita kwa mtaa wake katika kitongoji kilichopo Hampton, Georgia, Marekani Julai 15,2023 na kuwaua kwa kuwapiga risasi majirani wanne, wote wakiwa ni watu wazima.
Mauaji hayo yalianzisha msako uliomalizika Julai 16 mwaka huu huko Longmore akiuawa katika majibizano ya risasi katika kitongoji kingine yapata maili 15 (kilomita 25) kaskazini mwa Hampton.
Shambulizi hilo liliwajeruhi na maafisa watatu wa polisi, ambao wote wanatarajiwa wanaendelea na matibabu.
Longmore alikuwa na "shida ya kiakili" mnamo 2014, na kusababisha kulazwa hospitalini, mama yake Lorna Dennis, aliiambia WSB-TV Julai 16,mwaka huu.
Anasema mtoto wake "aliendelea kuzorota" lakini alikataa kutafuta matibabu, na kwamba maafisa walisema hawawezi kumlazimisha kutafuta huduma.
Anasema Longmore aliwahi kutumika katika Jeshi, alikuwa akiishi naye katika miaka ya hivi karibuni, na kwamba anatumai kuwa ndugu wa waathiriwa wangeweza kupata amani na Mungu.
Meya wa Hampton Ann Tarpley alitangaza Julai 16 mwaka huu kwamba jiji hilo lingefanya mkesha wa maombi Julai 17 mwaka huu  kutokana na tukio hilo lililochukua uhai wa watu wanne waliofariki katika jiji hilo la watu 8,000 ambao ni Scott Leavitt, 67, na mkewe, Shirley Leavitt, 66; Steve Blizzard, 65; na Ronald Jeffers, 66.
Risasi hizo ziliashiria mauaji ya 31 ya umati kwa 2023 nchini Marekani, na kuchukua maisha ya watu wasiopungua 153 mwaka huu, kwa mujibu  na kanzi data iliyohifadhiwa na The Associated Press na USA Today kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Northeastern.
Longmore aliuawa kama maili 15 (kilomita 25) kaskazini mwa Hampton katika kitongoji cha Jonesboro.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.